Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja jijini Dar Es Salaam mapema leo. Wengine pichani ni Meneja wa Ubora wa huduma kwa wateja, Mwangaza Matotola, Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal Kamouni na Mkuu wa kitengo cha uendesheji wa huduma kwa wateja Tigo, Zaeem Khan.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI,Nidal Kamouni akiongea na wanahabari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez (kushoto)na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal Kamouni wakikata utepe kuzindua kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja cha Tigo jijini Dar Es Salaam mapema leo.
Meneja wa Ubora wa huduma kwa wateja Tigo, Mwangaza Matotola akitoa maelezo ya jinsi ya uendeshaji wa kituo kwa mkurugenzi mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kituo hicho kipya cha huduma kwa wateja cha Tigo.
Timu ya watoa huduma kwa wateja wakionyesha jinsi ya utendaji wa kazi zao.

Kampuni ya Tigo Tanzania ambayo inaongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali leo imetangaza kufungua kwa kituo kipya cha kisasa cha huduma kwa wateja (Call Centre) kikiwa ni cha kwanza nchini Tanzania.

Ikiwa inajivunia teknolojia ya hivi karibuni kituo hicho cha miito kimetengenezwa ili kuwapatia wateja wa Tigo huduma ya daraja la juu duniani katika namna ambayo ni ya ufanisi na uhakika zaidi kutoka kwa mawakala wa huduma kwa wateja waliopata mafunzo ya hali ya juu.

Kituo hicho kipo kitalu namba 395 Ursino barabara ya Kawawa, Kinondoni jijini Dar es Salaam kikiwa kimesaidiwa Kundi la PCCI ambalo ni kiongozi wa soko katika uzoefu wa mteja na uendeshaji wa vituo vya huduma.

Akizungumza kuhusu kituo kipya cha miito ya simu wakati wa hafla ya kuashiria uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Diego Gutierrez alisema, “Uwekezaji wetu katika kituo hiki kipya cha miito ya simu kunaashiria kujituma kwetu katika kukua na kubadilisha mtiririko ambao tumekuwa tukitumia kuwafikia wateja wetu. Washirika wetu wa kibiashara na wateja binafsi hivi watarajie kupata huduma ya hali ya juu kwa mteja inayopatikana hapa nchini, ikiwa inatolewa na na mawakala wa kituo walio tayari kutoa huduma bora.”

Gutierrez alifafanua kuwa kituo hicho kipya kimefungwa teknolojia ya aina yake na miundombinu iliyo na usalama wa data utakaowezesha kulinda taarifa za wateja pamoja na utambulisho wao.

Aliendelea kuongeza kuwa kituo hicho kinajumuisha chumba cha mafunzo ambapo watu binafsi wanapigwa msasa ili kuwa mawakala wa kituo.

PCCI inaendesha shughuli zake katika maeneo 20 duniani ikiwa na wafanyakazi 7,000 ambao watakisaidia kituo cha Tigo Tanznaia katika kutoa jukwaa la kipekee katika uzoefu wa kuhamasisha wateja na kuwa na ukaribu nao. Ikiwa inajiweka katika mwenendo uliopo sasa PCCI itawapatia wateja wa Tigo sio tu huduma ya kawaida ya ya kuwasiliana na kituo bali pia suluhisho la jipya la kidijitali la huduma kwa mteja ambalo linajumuisha mtandao wa jamii kuchati kielektroniki na barua pepe.

“Tunafurahi kushirikiana na moja ya kampuni ya mawasiliano ya simu inayoongoza duniani, Tigo kama mshirika aliyechaguliwa kusimamia kituo chake cha mawasiliano nchini Tanzania. Uendeshaji wa kituo hiki kipya unashirikisha wataalamu wa ndani wa PCCI na na makao makuu yayake yapo Dubai. Kadhalika kama sehemu ya ushirikiano huu PCCI itaajiri zaidi ya watu 500 ili kusaidia vipaji vya ndani, “ alisema Ofisa Mtendaji Mkuu wa PCCI Nidal kamouni.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Tigo uendeshaji wa huduma za wateja, Zaeem Khan alithibitisha tena kujikita kwa kampuni hiyo ya mawasiliano ya simu katika kutoa teknolojia ya hali ya juu kwa wateja wake akibainisha kuwa kituo hicho kipya kwa mara nyingine tena kimeiweka Tigo katika nafasi ya kuongoza katika soko.

“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kwamba kupitia kituo miito wataendelea kupokea huduma za hali ya juu zisizo na kasoro kuwa na mawasiliano ya ana kwa ana na kushikamana na kuliko hai kutoka kwa timu zetu zilizopata mafunzo vizuri,” alisema Khan.

Khan alifafanua kwamba uwezo wa Tigo wa kujibadili kulingana na mabadiliko ya mahitaji ya wateja na matamanio yake yameiweza kutoa kwa ufanisi mkubwa hatua kwa hatua na hivyo kuifanya kusimama kivyake ndani ya soko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: