Sunday, April 30, 2017

UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI VYAIGIZA HASARA TANGA UWASA YA MILIONI 13 KWA SIKU

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusiana na mikakati waliochukua kukabiliana na kuondoa tatizo la maji machafu yanayotoka jijini Tanga ili kuhakikisha maji yanarudi kwenye hali yake
ya kawaida lakini kulia ni Meneja wa Ufundi wa Mamlaka hiyo,Farles Aram
Kushoto mwenye tisheti ya njano ni Mwandishi wa Gazeti la Majira Mkoani Tanga,Mashaka Mhando akiuliza swali katikati ni Joachim Kapembe kutoka Shirika la
Utangazaji la TBC na kulia ni Mwandishi wa ITV na Radio One Mkoani Tanga, Wiliam Mngazija.
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony kulia akiuliza swali kwenye mkutano huo kushoto ni Mwandishi Zawadi Kika wa Clouds TV
Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorrah Killo kulia ni Mwandishi wa Gazeti la Citizeni George Sembony
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya watumishi wa mamlaka hiyo wakifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari
Waandishi wa Habari Mkoani Tanga wakichukua habari
Waandishi wa habari wakitazama namna maji yaliyohifadhiwa kwenye kituo cha kusafishia maji cha Mowe kabla ya kufika kwa walaji wa kwanza ni Sophia Wakati wa Gazeti la Uhuru wa pili ni Mbaruku Yusuph wa gazeti la Tanzania Daima
Mwandishi wa Gazeti la Mtanzania, Sussan Uhinga naye akiangalia namna maji yanavyosafishwa kabla ya kuwafikia walaji
Waandishi wa Habari wakiongozwa na Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania wakitembelea eneo la kusafishia maji kabla ya kufika kwa watumiaji la
Eneo la Mowe ambalo maji huchujwa kabla ya kuwafikia walaji
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati walipoitembelea kujionea.
William Mngazija wa ITV na Radio One Mkoani Tanga akiwa ongoza waandishi wengine kuingia kwenye vyanzo vya maji kuona namna hali ilivyo
Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony akiwa kwenye vyanzo
hivyo vya maji
Muonekano wa Maji kwenye chanzo cha Maji cha Mto Zigi

MAMLAKA ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye vyanzo vya maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika maeneo hayo.

Mhandisi Mgeyekwa alisema shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika.

Aidha alisema kuwa awali mamalaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya Jiji la Tanga.

Mkurugenzi huyo alisema tayari mamlaka hiyo imekwisha kuanza kuchukua jitihada za haraka ikiwemo kutumia maji ya kisima cha mwakileo ambacho kina uwezo wa kutoa maji kwa ujazo wa km 30,000 hadi 35,000 ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya zaidi wananchi 47,000 kwa wakati mmoja sambamba na kuzibua mabomba ambayo yamekuwa na tope iliyosababishwa na mvua zinazoendelea sasa.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha madhara makubwa kwa watumiaji wake ikiwemo kupungua kina cha maji na maji kutoka machafu jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu