Jeshi la Polisi limewakamata Jumla ya watuhumiwa 267 kwa Makosa mbali mbali ya kihalifu pamoja na Madawa ya kulevya, Unyang'anyi wa kutumia Silaha katika Maeneo Mbali Mbali ya Jiji La Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda Polisi kanda Maalum Dar es salaam Saimon Sirro amesema Operation hii ni endelevu na Jumla ya kete 366 za dawa zakulevya zimekatwa pamoja puli za bangi 150 na Misokoto ya bhangi 51.

Aidha Sirro amesema kuwa Operatini Kali ya kuwasaka wahalifu wa Makosa hayo mbali mbali ikiwemo kosa la kupatikana na Madawa ya kulevya bado inaendelea na hivyo tunawaomba raia wema waendelee kutoa Ushirikiano mzuri kwa Jeshi la Polisi ili kufanikisha kukamatwa kwa waalifu.
" Watuhumiwa wote kwa ujumla bado wanaendelea Kuhojiwa Kulingana na Makosa Yao na pindi Upelelezi Utakapokamilika Watafikishwa Mahakamani kwa hatua nyingine zaidi" amesema Sirro.

Pia Kamishna huyo ameongeza kuwa mnamo tarehe 15 Mwezi huu 2017 Majira ya Saa moja Usiku Maeneo ya kiwalani kwa Ally Mboa Jeshi la polisi limefanikiwa kukamata Silaha Moja aina ya Shotgun ambayo imekatwa kitako na Mitutu na huku namba zake zikiwa zimefutwa.

"Siraha hiyo ilipatikana wakati Askari wakiwa doria katika Maeneo hayo ambapo Waliskia harufu ya bangi na Kuanza kufuatilia ili kubaini ilipokuwa ikitokea na ndipo Ghafla watu wawili wasiofahamika walikurupuka na kupanda pikipiki ambayo haikusomeka namba kisha kuangusha begi moja la mgongoni ambalo lilikuwa na Silaha" amesema Sirro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: