Mkulima mmoja alikuwa na Punda ... Punda aliyedumu nae kwa miaka mingi sana aliyemsaidia shughuli za kilimo na uchukuzi..alikaa naye toka akiwa mtoto mpaka punda akawa mzee kabisa.

Siku moja wakiwa wanatoka shambani, kwa bahati mbaya yule punda alitumbukia kwenye kisima kirefu sana ambacho kwa wakati ule kilikuwa kimekauka.

Yule Mkulima akawaza sana atafanyaje kumtoa yule punda..na baada ya kutafakari sana akasema kwanza hata hivyo huyu punda ameshazeeka ni hasara kuingia gharama za kumtoa...akaona vema tu amzike humo humo

Akaenda kuita majirani ,wakaja na sepetu wakaanza kumwagia udongo, mchaka na kokoto shimoni kumfukia.

Mwanzoni tu ni kama punda alijua kinachoendelea..akapaza sauti na kulia kwa sauti kali ajabu..sauti ya malalamiko...hawakujali waliendelea kufukia..kwa kutupia kila aina ya taka taka

Baadae kidogo kwa mshangao wa wengi ghafla punda alinyamaza kimya kabisa sauti ikapotea....baada ya kutupia taka kadhaa..mkulima yule akaamua kuchungulia shimoni....Alistushwa mno na alichokiona

Kila taka na mchanga ulipokuwa ukiangukia mgongoni mwa punda...alikuwa akifanya kitu cha kushangaza.

Kila udongo ulipomwangukia..alijitingisha ukamwagika na akaukanyaga akainuka juu kidogo...kila ulipokuja aliendelea kufanya hivyo hivyo..hatimaye baada ya Muda mkulima na majirani walishangaa kuona amefika juu kabisa ya ukingo wa kisima na akatoka kwa furaha kabisaa.

Kuna wakati maisha yanakurushia matakataka ya kila aina,acha kulia na kupiga kelele, jitingishe...yafanye ngazi..Kila jaribu linalotupata ni ngazi ya kupandia.

Kamwe hatuwezi toka kwenye visima virefu kwa kulia peke yake..bali kwa kupambana kuchomoka.

Wacha waone uko kimya baada ya makombora waliokurushia...yatake yapange..yafanye ngazi ya kupandia...

Changamoto yeyote unayopitia sasa...ni shimo na michanga..sisi ni zaidi ya punda..acha kulia, jikung`ute, yakanyage ,nyanyuka juu, toka Kanyaga Twende
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: