Wednesday, May 3, 2017

EATV WAZINDUA SHINDANO LA MPIRA WA KIKAPU 'BBALL KINGS' LITAKALOANZA MAY 15, 2017 JIJINI DAR

 Meneja Mauzo na masoko wa EATV , Roy Mbowe (katikati) akiongea na waandishi wa habari leo wakati akitangaza kuanza kwa shindano la mpira wa kikapu linalokwenda kwa jina la 'Bball Kings, (pembeni kulia) ni  mwakilishi wa kampuni ya Coca-Cola nchini, Pamela Lugenge na Mwakilishi wa TBF, Mwenze Kibinda.
Mwakilishi wa kampuni ya Coca-Cola nchini, Pamela Lugenge akiongea jinsi kampuni ya Coca-Cola atakavyodhamini kupitia kinywaji cha Sprite. Picha na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Kituo cha televisheni cha EATV kimeandaa mashindano ya mpira wa kikapu yatakayo kwenda kwa jina la 'Bball Kings' ambayo yatajumuisha timu zote za mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es Salaam leo Meneja Mauzo na masoko wa EATV , Roy Mbowe amesema kuwa mashindano hayo ambayo yanataraji kushirikisha timu tofauti kutoka nchi ya Tanzania na kufanyika katika viwanja tofauti vya jiji la Dar es Salaam.

“Dhumuni la Mashindano haya ni kutangaza na kuibua vipaji vipya vya michezo wa kikapu hapa nchini hivyo tayari tushapata kibali kutoka shirikisho la mpira wa kikapu nchini (TBF)” amesema Mbowe.

Ametaja kuwa mashindano haya yatakuwa na hatua kuu saba kuanzia hatua ya usahili, warsha, Kufuzu, kuminasita bora, Robo fainali, Nusu fainali na Fainali.

Ametaja kuwa mshindi wa mashindano hayo ataweza kujinyakulia zawadi ya shilingi Milioni kumi pamoja na kombe la ubingwa na kutaja kuwa mshindi wa pili atapewa milioni tatu na mchezaji bora kupewa milioni 2.

Mbowe ametaja kuwa vigezo vya kushiriki mashindano hayo ni vijana wa kiume pekee hivyo watu wataruhusiwa kuunda timu zao za mtani na kila kikosi kitaruhusiwa kuwa na wachezaji wasiozidi 3 kutoka timu za daraja la kwanza na kutaja kuwa timu inatakiwa isipungue wachezaji 10 .

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu