Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Bima ya AAR, Tabia Masoud ( kulia) akizindua huduma ya Aplikesheni mpya ya simu ili kusaidia wateja kupata huduma bora za afya, kushoto ni Meneja mauzo msaidizi wa huduma mbadala wa kampuni hiyo, Jumanne Mbepo. Katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam leo.
Meneja Mauzo Msaidizi wa huduma mbadala wa Kampuni ya Bima ya AAR, Jumanne Mbepo (kulia) akizungumza na waandishi jijini Dar es salaam wakati akizindiua mpango wa bima wa afya kwa wanafunzi ujulikanao kama AAR Inshule. Kushoto ni Meneja Mkuu wa huduma kwa wateja Esther Swai.

Kampuni binafsi ya Bima ya afya inayoongoza nchini Tanzania, AAR imefanya uzinduzi wa Aplikesheni mpya ya simu ili kuwawezesha wateja kupata huduma mbalimbali kupitia simu zao.

Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya Bima ya AAR , Tabia Masoud alisema katika mkutano na waandishi wa habari leo kwamba, Aplikesheni hiyo kwa sasa inapatikana kwenye simu zenye mfumo wa android na hivi karibuni itakuwa ikipatikana katika mfumo wa IOS. Alisema aplikesheni hiyo ya simu ina kazi nyingi muhimu ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wateja na watoa huduma za matibabu walioko kwenye mtandao wa AAR ili kurahisisha huduma za afya.

“Tunafuraha kuzindua aplikesheni hii mpya ya simu ikiwa ni sehemu ya thamani tunayo muongezea mteja kwasababu lengo kuu katika mkakati wetu wa biashara ni kutoa huduma inayokidhi mahitaji ya wateja. Kipaumbele kikubwa cha wateja wetu nikupata huduma za afya haraka iwezekanavyo kutoka kwenye mtandao wetu ambapo matitabu hutolewa kwa kutumia bima badala ya fedha taslimu na vilevile ni kipaumbele chao kudai kurudishiwa fedha zao pale ambapo wanapata matibabu kwakulipia. Aplikesheni yetu mpya itawasaidia wateja kupata taarifa za huduma katika hospitali mbalimbali zilizopo kwenye mtandao wetu, kwasababu hiyo, sasa mteja anaweza kufanya mawasiliano mapema na kupewa muda maalum wa kwenda hospitali, vilevile aplikesheni hii itawasaidia wateja kujua taarifa mbalimbali za kuhusu bima zao muda wowote ule”.

Wakati huohuo, Kampuni ya Bima ya Afya ya AAR imezindua mpango wa bima ya Afya kwa wanafunzi ujulikanao kama AAR Inshule, mpango huo umeundwa ili kuboresha ustawi na afya ya wanafunzi nchini kote.

Meneja mauzo msaidizi wa huduma mbadala wa kampuni hiyo, Jumanne Mbepo alisema kwamba Inshule itawawezesha wanafunzi kunufaika na huduma mbalimbali za matitabu ikiwa ni pamoja na Huduma ya Matibabu ya Kutwa, Matibabu ya Kulazwa, huduma ya macho, huduma ya meno,msaada wa vifaa vya matibabu na huduma za matibabu ya Akili. Mpango huo wa bima ya afya pia unatoa malipo ya mkupuo kwa familia katika kipindi cha mazishi ya mwanafunzi.

Bima ya Inshule itapatikana kwa wanafunzi wote nchini Tanzania na itakuwa ikiuzwa kupitia uongozi wa Shule zao .Bima hii inalenga kusaidia wanafunzi Kupata matibabu sahihi na ya haraka hususani wakati wa dharura kupitia mtandao wa watoa huduma zamatibabu wenye Mikataba na AAR.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: