Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 amefanya mazungumzo na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam wakifatilia  kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017
Mkurugenzi wa Manispaa ya ubungo Ndg john Lipesi Kayombo akifatilia kwa makini maelekezo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda Leo Mei 18, 2017 wakati wa kika na Watendaji wa Sekta ya Ardhi Na Ujenzi kutoka Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda akisisitiza jambo.
Na Mathias Canal, Dar es Salaam.

Imebainika kuwa zipo kauli zisizo rafiki zinazotolewa na watumishi wa Umma dhidi ya wananchi katika Jiji la Dar es salaam wanaozuru katika Ofisi mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali kutokana na mambo yanayowakabili.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul C. Makonda amebainisha hayo leo Mei 18, 2017 wakati akizungumza na watendaji wa Sekta ya Ardhi na Ujenzi wanaohudumu katika Manispaa za Ubungo, Kigamboni, Kinondoni, Temeke, Ilala Na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam ambapo pia ametoa maelekezo 17 ya kuzingatia katika utendaji wao.

Mhe Makonda amesema kuwa mtumishi wa serikali ambaye atabainika kutumia lugha ambazo sio rafiki kwa wananchi atachukuliwa hatua za kinidhamu mara baada ya kubainika kwani kufanya hivyo ni kufifisha uaminifu wa wananchi dhidi ya serikali.

Sambamba Na hayo pia RC Makonda amesema kuwa kazi ya watendaji serikalini ni kutatua kero za wananchi japo wapo watendaji ambao wamegeuka na kuanza kuongeza migogoro badala ya kutatua.
Alisema kuwa baadhi ya watumishi wa Sekta ya ardhi wanamiliki kampuni zinazojihusisha na mambo ya Ardhi jambo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa likipunguza ufanisi katika utendaji kwani wanatumia muda mwingi kufikiri kuhusu kampuni zao kuliko kuwatumikia wananchi serikalini.

Ametoa wiki moja kwa watumishi wote wanaomiliki kampuni hizi kuamua moja ama kubali wakifanya kazi serikalini na kuachana na kampuni binafsi ama kubakia katika kampuni zao Na kuacha kazi serikalini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: