Kaishna wa Bima nchini Dkt. Baghayo Saqware akiwa anazungumza na wauza bima,madalali wa bima, mawakala wabima, wauza bima, jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani, viongozi wa vyama vya wamiliki wa mabasi pamoja na umoja wa waendesha pikipiki.Picha na Vero Ignatus Blog.
Meneja wa Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Kanda ya kaskazini Eliezer Rweikiza akizugumza katika uzinduzi huo wa uhakiki wa Bima kwa njia ya simu ya mkononi, uliofanyika Jijini Arusha leo, wa kwanza kulia ni Kamishna wa Bima Taifa Dkt. Baghayo Saqware, akifuatiwa na aliyepo kulia kwake ni Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman.
Meneja waTEHEMA kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima(TIRA), Aron Mlaki akiwa anawonyesha namna ya kutambua Bima kama ni halali au ni feki kwa kutumia simu ya mkononi.
Baadhi ya washiriki mbalimbali waliohudhuria kwenye uzinduzi huo mfumo wa kuhakiki Bima kwa njia ya simu ya mkononi.
Mwanasheria wa Mamlaka ya usimamzi wa Bima (TIRA), Arthur Mbena akiwa anawaelekeza wa kikosi cha usalama barabarani namna ya kutambua Bima kama ni halali au feki kupitia simu ya mkononi kwenye gari kama linavyoonekana pichani.
Meneja wa TEHAMA kutoka Mamlaka ya Usiamizi wa Bima(TIRA)Aron Mlaki akitoa elimu kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani namna ya kutambua Bima feki au halali ,ni ya kampuni gani, Bima gari la matumizi gani, aina gani ya bima kubwa au ndogo.

Na Vero Igantus, Arusha.

Mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini(TIRA)imezindua mfumo wa uhakiki wa Bima kwanjia ya simu za mkononi kanda ya Kaskazini ambapo zoezi hilo limeambatana na ukaguzi wa bima kwenye vyombo vya moto na kubaini bima feki katika baadhi ya magari na pikipiki.

Akizindua mfumo huo kwa kanda ya kaskazini uliofanyika jijini Arusha Kamishna wa Bima Nchini Dkt.Boghayo Saqware amesema kuwa kampeni yao ina laengo la kuondoa bima feki sokoni ambazo zinazouzwa ama kutengenezwa na wahalifu, ambalo kwa mujibu wa sheria wanafanya kosa la jinai.

“Tumeanzia Pwani na sasa tupo Arusha na zoezi hili litakuwa endelevu, kwahiyo tunawaasa wananchi wanunue bima halali,tumezindua mfumo ambao ni rahisi kwa mtu anaenunua bima kujihakikishia kuwa bima hiyo ni feki au halali .”alisema Dkt. Baghayo.

Kamishna huyo amesema kuwa kwa miaka ( 3) kesi (10) za Bima feki ziliamuliwa, watu (5) walihukumiwa kifungo jela, (2) wamelipa milioni 20,000,000, hadi 40,000,000, mashauri ya jinai yaliyopo mahakamani yalifunguliwa mwaka 2016 Mbeya (1) Mafinga (2) Mara (1) na Dar es salaam (3) na kufikia jumla ya kesi mpya 7, ambapo mashauri yaliyopo kwenye uchunguzi wa polisi ni (10).

Kwa upande upande wake Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Kanda ya kaskazini Eliezer Rweikiza amesema kuwa zoezi hilo katika Jiji la Arusha litaendelea kwa wiki nzima ambapo wataelekea Kilimanjaro, Tanga ambapo amesema kuwa 10% ya magari hapa nchini Tanzania hayana Bima halali,amesema hadi sasa hapa nchini kuna makampuni 31 ya Bima, mawakala 500 madalaliwa Bima ni zaidi ya 100.

“Kuna mtu akienda kukata Bima anakuwa hajui kuwa hiyo ni feki,na kuna mwingine aknajua kuwa hiyo ni feki na nashirikiana na yule anayemkatia,hivyo akibainika anafutiwa leseni mkatajia halafu taratibu nyingine za kisheria zinafuata kwani kwa utafiti ulikwisha kufanyika Jiji la Arusha ni la pili kwa kuongoza kwa pima feki huku Jiji la Dar es salaam kinara” alisema Rweikiza.

Naye meneja wa Tehama Aron Mlaki (TIRA)ameelezea namna ambavyo mtu anaweza kuhakiki Bima kwa njia ya simu ya mkononi ambapo amezitaja njia kuu mbili ambazo ni inaweza kuwa kwa intaneti au njia ya ujumbe mfupi wa maneno.

Kwa njia ya ujumbe mfupi (unaandika maneno stika unaweka namba ya bima kwa tarakimu zisizozidi 7 unatuma kwenye namba 15200 na hii ni kwa mitandao ya Vodacom na Tigo peke yake.”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: