Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Meneja Masoko Msaidizi wa Coca-Cola,Pamela Lugenge,akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa michezo ya Umisseta Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule zitakazoshiriki mashindano ya UMISSETA Copa Coca-Cola wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla pamoja na maofisa wa kampuni ya Coca-Cola wakipasha mwili kwa mazoezi kabla ya uzinduzi wa mashindano hayo.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla akikagua baadhi ya timu za wanafunzi wakati wa uzinduzi wa mashindano ya UMISSETA Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mwishoni wa wiki
Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondari wakifanya mazoezi kwa kushirikiana na wachezaji wa Mbeya City wakati wa uzinduzi wa mashindano ya Copa Coca Cola katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya mwishoni mwa wiki.
Wanafunzi wakionyesha umahiri wa kusakata kabumbu wakati wa uzinduzi wa mashindano katika uwanja wa Sokoine mwishoni mwa wiki.
---
Michezo ya Umoja wa Michezo ya Shule za Sekondari-UMISSETA Copa Coca- Cola kwa Mkoa wa Mbeya imezinduliwa rasmi mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Sokoine na uzinduzi huo ulionogeshwa na wachezaji wa timu ya soka ya Mbeya City ambao walishiriki kufanya mazoezi na timu za wanafunzi na kutoa ushuhuda wa michezo hiyo ilivyoibua vipaji vyao.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Amos Makalla,ambaye alikuwa mgeni rasmi anataka kuwaona vijana wengi wakishiriki mazoezi na michezo mbalimbali kwa kuwa michezo kama ilivyo hii ya UMISSETA Inaibua na kukuza vipaji pia sekta ya michezo bado inazo fursa nyingi za kujiajiri.

Alisema kampuni ya Coca- Cola imeonyesha njia kwa kudhamini michezo hii na kutoa wito kwa makampuni mengine kujitokeza kudhamini michezo ya vijana kwa kuwa ndio tanuru la kuwaandaa wachezaji na kuibua vipaji.

‘’Leo hii tunaona hawa vijana wa Mbeya City wapo hapa kutoa ushuhuda wao, wanapokea mpunga (mshahara) wa maana lakini chimbuko lao wametokea kwenye michezo hii ya Copa Coca- Cola. Naamini kupitia michezo hii Mbeya tutapata wachezaji wengi zaidi’.Alisema.

Ofisa Msaidizi Masoko wa Coca- Cola Pamela Lugenge, alisema lengo la kampuni ya Coca Cola kuuungana na Serikali kupitia UMISSETA ni kuona wanaibua vipaji vingi vya vijana walioko shule za sekondari ambako wanaamini ndiko chimbuko la kupata timu ya taifa na klabu mbalimbali nchini.

“Tumeamua kuanzia kwenye mizizi ngazi ya chini kabisa, tunaamini huku ndiko vipaji viliko lala, tunataka kuibuwa akina Mbwana Samata wengi zaidi kuanzia huku, ndio maana tumejikita zaidi, na tunagawa vifaa vya michezo kwa shule zote, tumeanza na shule hizi 39 za jiji la Mbeya na baada ya uzinduzi huu sasa tunakwenda kwa wilaya zote kutoa vifaa hivi,” alisema Lugenge.

Mchezaji wa Mbeya City, Medson Mwakatundu,akiongea kwa niaba ya wachezaji wenzake walioibuliwa na UMISSETA alisema michezo hii ni muhimu sana iwapo Tanzania tunataka kuwa na wanamichezo wazuri kwa kuwa inaibua na kukuza vipaji na alitoa wito kwa vijana kushiriki michezo kwa kuwa inazo fursa nyingi za ajira na kutangaza taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: