Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, (CCM) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Solwa kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga alipotembelea zahanati ya Solwa kisha kukabidhi msaada wa viti viwili vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,viti viwili kwa ajili ya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia kwa akina mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kumkabidhi Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim (kulia) vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia akina mama (alivyoshikilia Dkt. Ibrahim )
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Solwa Emmanuel Ngamba wakati akikabidhivitanda vya kujifungulia,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika kwenye chumba cha kujifungulia akina mama
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia
Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Hellena Daudi akiwa na baadhi ya madiwani wa CCM wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba katika zahanati ya Solwa
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba katika zahanati ya Solwa
Diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh akielezea matatizo yanayokabili wananchi wa kata hiyo
Wazee wa kata ya Solwa wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amebeba mtoto katika chumba kinachotumika kama wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo aliahidi kutoa mabati 20 kusaidia ujenzi huo ambao umetokana na nguvu za wananchi walioamua kuchangishana pesa na kuanza kujenga ili kukabiliana na changamoto ya vifo vya akina mama na watot
Ndani ya chumba cha lishe-Mheshimiwa Azza Hilal Hamad na diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh wakiangalia chakula dawa (unga maalum wenye lishe) 'Multiple Micronutrient powder) kinachotolewa kwa watoto wenye utapiamlo wanaofika katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amembeba mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati ya Solwa baada ya mzazi wake Grace Richard (kushoto) kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akimweleza mama wa mtoto huyo kuwa ameguswa na hali ya mtoto huyo ambaye afya yake siyo nzuri hivyo kuahidi kutumia mbinu mbalimbali ili mtoto aweze kufanyiwa huduma ya upasuaji
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha mheshimiwa Azza Hilal Hamad vyeti vya mtoto Salawa Mihangwa anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati ya Solwa ambayo sasa inalea watoto 95 wenye tatizo la utapiamlo huku mtoto anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo akiwa mtoto wa kwanza kulelewa katika zahanati hiyo
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na akina mama wenye watoto wanaolelewa katika zahanati ya Solwa kutokana na watoto kukabiliwa na utapiamlo ambapo aliwasisitiza kuwapatia watoto mlo kamili na kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa masuala ya afya
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akigawa matunda kwa watoto wanaopata huduma ya lishe katika zahanati ya Solwa

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimia Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ametembelea Zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoa wa Shinyanga kisha kutoa msaada wa viti vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia na viti vya wagonjwa (wheel chairs) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.

Vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa tiba alivyovipata kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Shinyanga.

Akitoa msaada huo jana Alhamis May 11,2017 Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema msaada huo utasaidia katika kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa kuwarahishia akina mama kupata huduma karibu badala ya kutembea umbali kufuata huduma za afya.

“Mimi ni mama nazifahamu changamoto wanazokabiliana nazo akina mama,nilitafakari na kuangalia nani wa kuweza kutusaidia,nikaenda ubalozi wa China nchini kuomba wasaidie akina mama wa Shinyanga,walikubali na leo nimeleta vitanda vya kisasa kwa ajili ya akina mama,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia”,alieleza Hamad.

Katika hatua nyingine mbunge huyo aliwapongeza wananchi wa Solwa kwa kujitolea na kuanza ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo ameahidi kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya paa la jengo hilo.

Aidha aliwataka wananchi kuachana na tabia ya kuwaozesha watoto wa kike na badala yake wawatafutie shughuli zingine za kufanya wanapofeli mtihani wa darasa la saba kwani wakiolewa wangali wadogo husababisha wapoteze maisha wakati wa kujifungua hivyo kuchangia ongezeko la vifo vya mama na mtoto katika jamii.

Mheshimiwa Hamad pia aliahidi kutafuta namna ya kumsaidia mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa na kupatiwa huduma za kiafya katika zahanati hiyo baada ya mzazi wake Grace Richard kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo katika zahanati ya Solwa, ametuletea picha 25 za matukio yaliyojiri,Tazama hapa chini
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: