Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewataka wadau wa afya mkoani Shinyanga kufanya kazi kwa uwazi ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza wanapotekeleza majukumu yao katika jamii.
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akimkaribisha mgeni rasmi,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Wadau wa afya wakiwa ukumbini.
Kikao kinaendelea.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizungumza ukumbini.
Kikao kinaendelea.
Kikao kinaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Telack ameyasema hayo leo Jumanne May 30,2017 wakati akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Telack alisema ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ni vyema wadau wakatekeleza majukumu yao kwa uwazi lakini pia taasisi na mashirika mbalimbali kujitambulisha serikalini kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika jamii.

“Mkoa wa Shinyanga una wadau wengi wa afya,naomba mfanye kazi kwa uwazi na kuzingatia maadili,lakini pia ni vyema kabla hujaanza kutekeleza mradi jitambulishe kwa viongozi wa serikali”,alieleza Telack.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alimtaka mganga mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua tahadhali kuhusu tishio la ugonjwa wa Ebola kwani wilaya hiyo ina mwingiliano wa watu wengi na wataalam wa afya wahakikishe wanatoa taarifa mara moja endapo mtu yeyote atabainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.

“Ugonjwa huu umeripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Congo ,hapa kwetu bado hatujapata taarifa za kuwepo mgonjwa wa ebola,niwaombe pia wataalam wa afya maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga kuchukua tahadhali juu ya ugonjwa huu”,aliongeza.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume aliwaondoa hofu wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuwa ugonjwa huo haujaingia mkoani humo na kuongeza kuwa tayari wameanza kuchukua tahadhali juu ya tishio la ugonjwa huo.

Dkt. Mfaume alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa afya kujitokeza kusaidia katika masuala ya dharura yanapojitokeza badala ya kujikita katika sera za taasisi ama mashirika wanayofanyia kazi.

Naye Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela alisema lengo la kikao hicho cha siku mbili cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga ni kuwaleta pamoja wadau wanaoshughulika na masuala ya afya ili kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya afya na namna ya kuzitatua lakini pia kufahamiana.

Miongoni mwa wadau waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na viongozi ngazi ya mkoa,halmashauri za wilaya, Shirika la Intrahealth International, CUAMM, Save the Children, JHPIEGO ,TAWLAE, Red cross, AGPAHI, World vision, ICS, PSI, AGAPE, Pathfinder International, Good Neighbors, USAID, TAMA, IMA, Amref International, HPSS na wengine wengi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: