Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakisiliza mafunzo elekezi ya viongozi wa mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Kimanta wakisikiliza mafunzo ya viongozi wa Mkoa wa Arusha yaliyotolewa kwa lengo lakukuza uwelewa.
Kutoka kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha Mh: Calist Lazaro pamoja na viongozi wa Mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo elekezi kwa viongozi wa mkoa wa Arusha.

Na Imma Msumba, Arusha

Viongozi wa Mkoa wa Arusha wameshauriwa kuwajibika katika majukumu yao huku wakifuata kanuni na sheria mbalimbali za utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi katika maeneo yao ya kazi huku wakileta maendeleo kwa mkoa.

Akifungua mafunzo elekezi kwa viongozi hao Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema viongozi wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuongeze mahusiano katika maeneo yao ya kazi baina yao na watumishi wachini yao.

Amesema lengo kubwa nikuondoa migongano inayojitokeza baina ya viongozi na watumishi hao ambayo inapelekea kudhorotesha utendaji wa kazi katika maeneo yao na kuongezeka wimbi la uwonevu kwa watumishi wao.

Aidha amewataka viongozi hao wasimamie uwajibikaji wa watumishi katika maeneo ya kazi kwa kufuata taratibu za majukumu yao.

Akisisitiza zaidi kwa kuwataka viongozi kutekeleza maelekezo yanayotolewa na ngazi za juu serikalini kwani mengi yanakuwa ni miongoni mwa shughuli zao za kila siku na hii itaongeza utii kwa viongozi serikalini.

Nae katibu tawala wa mkoa Richard Kwitega amesema mafunzo hayo niyakukumbushana majukumu kwa viongozi hao huku wakipitia maeneo mbalimbali ikiwemo wajibu na majukumu ya viongozi,usimamizi wa Rasilimali watu sehemu za kazi napia kupitia kanuni na maadili ya viongozi na utumishi wa umma.

Amesema mafunzo hayo yatakuwa ya siku 2 huku yakishirikisha baadhi ya viongozi kutoka TAMISEMI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: