Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mgeta kilichopo Wilaya ya Mvomero mkoani humo Masumbuko Igembya, ili kupisha uchunguzi kufuatia tuhuma za kujihusisha na ubadhirifu wa fedha za mfuko wa afya ya Jamii (CHF).

Wakati huo huo Dkt. Kebwe ameagizwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria maafisa waandikishaji 12 wa mfuko wa CHF kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, mara baada ya kushindwa kuwasilisha kiasi cha Shilingi Milioni 1.5 walizokusanya kutoka kwa wananchi, kwa lengo la kuwaunganisha katika mfuko wa afya iliyoboreshwa.

Dkt. Kebwe amechukua uamuzi huo, wakati akiwa katika ziara yake ya kujionea uendeshwaji wa Mfuko wa afya ya Jamii, Katika Halmshauri za Mvomero na Mnispaa ya Morogoro iliyolenga kubaini changamoto zinazoukabili mfuko huo.

Akiwa Wilayani Mvomero anakutana na changamoto ya ukusanyaji na usimamizi mbovu wa fedha zinazotolewa na wananchi kwa ajili ya mfuko huo, kwani kiasi kilichokusanywa ni Shilingi 19,000 pekee kwa kituo cha afya cha mgeta, hali inayomlazimu kuchukua hatua.

Baada ya kutoka Mvomero anahamia katika halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, ambako nako nako anakuta waliopewa dhamana ya kukusanya michango ya CHF wameshindwa kuifikisha sehemu husika.

Pamoja na maagizo hayo, Dkt. Kebwe ametoa miezi mitatu kwa Waganga Wakuu wa Wilaya zote mkoni hapa, kuhakikisha kila mmoja anafikia asilimia 20 ya makusanyo ya fedha za mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa na ambaye hatafikia asilimia hiyo atachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: