Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza katika Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisaini kitabu cha wageni Mara baada ya kufika Shule ya Msingi Ubungo Plaza kwa ajili ya Mkutano uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akikagua Mipaka ya eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkutano  uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Kaimu Mkurugenzi ambaye pia ni Afisa Utumishi Mkuu Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally akijibu baadhi ya maswali ya wananchi wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017 
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Ally, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo Na Ofisa Mtendaji wa Kata Ya Ubungo Ndg Isihaka Waziri wakisikiliza Maelezo kuhusu Shule ya Msingi Ubungo Plaza kabla ya Mkuu wa Wilaya kuzuru shuleni hapo kwa ajili ya Mkutano
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori wakati wa Mkutano uliofanyika katika Shule ya Msingi Ubungo Plaza uliowajumuisha walimu, Mtendaji, Wajumbe wa Mitaa, na wananchi. Leo Mei 19, 2017

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 19, 2017 ameagiza kujengwa madarasa nane mapya katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam kutokana Na uchakavu wa Majengo ya madarasa yaliyopo sasa.

Ametoa agizo hilo katika mkutano wake na uongozi wa shule hiyo ukiwajumuisha mtendaji na wajumbe wa mitaa,walimu na wananchi ambao waliohudhuriwa katika viwanja vya shule ya Msingi Ubungo Plaza.

Mhe Makori amesema kuwa ili kuboresha elimu katika Wilaya ya Ubungo ni wazi kuwa ni lazima kuwe Na miundombinu rafiki kwa wanafunzi wanapokuwa darasani kwa ajili ya masomo kwani ubovu wa Majengo ya shule,ubovu na uhaba wa vyoo ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wanafunzi kufeli kutokana na kutokuwa Na miundombinu rafiki.

Alisema kuwa Kodi zinazokusanywa Na serikali kwa wananchi ni kwa ajili ya kuwaimarishia miundombinu kuboresha afya, na Elimu hivyo serikali ni lazima ishughulikie na Kusimamia shughuli zote ikiwemo Ujenzi wa madarasa kwa manufaa ya wanafunzi Na wananchi kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ametoa maagizo hayo Wakati akijibu Risala iliyosomwa Na Mkuu wa Shule ya Msingi Ubungo Plaza Bi Theresa Masaba ambayo ilibainisha changamoto nyingi ikiwemo Ukosefu wa Vyoo Bora, Ukosefu wa Uzio, Uchakavu wa Majengo ya shule, Upungufu wa Majengo (Ofisi ya Walimu, Darasa la awali Jiko, Maktaba), Maji taka kuelekezwa kwenye eneo la shule, Eneo la shule kufanyika kama sehemu ya kuvutia bangi Wakati wa jioni na siku za Wikendi sambamba na Upungufu wa samani za shule.

Mhe Mkuu wa wilaya ameagiza pia kuvunjwa kwa Vyoo vilivyopo Na kujengwa Vyoo vingine vipya sambamba na kujengwa kwa uzio wa shule ili kuepuka kadhia ya watu wanaotumia kama Eneo la kuvutia bangi Na vitendo vingine viovu visivyo kubalika katika jamii.

Aidha amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha anawakamata watu wote wanajihusisha Na uvutaji bangi katika Eneo la shule kwani Jambo hilo halikubaliki si tu Na shule hiyo Bali Na serikali kwa ujumla.

Sambamba Na hayo pia Mkuu wa wilaya ameagiza kuvunjwa kwa ukuta wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) ambapo Uzio wake umejengwa ndani ya Eneo la shule.

Alisema kuwa Kanisa hilo tayari lilishapewa Notisi ya siku Saba tangu Mei 8 mwaka huu kwa ajili ya kuvunja ukuta huo lakini hawakufanya hivyo.

Akitoa salamu za shukrani kwa niaba ya Walimu Na wanafunzi wa shule, Mwenyekiti wa kamati ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza Ndg Ramadhani Maughuu amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kutembelea shule hiyo Na kutatua changamoto hizo zilizokuwa zinaikabili shule hiyo kwa muda mrefu.

Maughuu ametoa pongezo zake pia kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda kwa ufanisi Na uchapa Kazi wake sambamba Na pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli kwa weledi Na ufanisi wa kuwahudumia watanzania Na kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: