Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Kinondoni na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mzimuni, ambaye pia ni Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali (kulia) akicheza muziki na Katibu Mwenezi wa Kinondoni, Mwinyimku Sangaraza, wakifurahia hotuba ya Naibu Katibu MKuu Bara baada ya kuwahutubia katika Jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam, jana. Picha Zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO).
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Matiku Makori, akizungumza kutoa tathmini ya usalama wa kisiasa katika Wilaya yake mbele ya mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, aliyekuwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama katika Jimbo la Ubungo, jijini Dar es Salaam, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa, Mabalozi na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akiwatambulisha Wenyeviti wa Serikali ya Mtaa na Mabalozi wa Kata ya Manzese na kuwapa majukumu baada ya kuzungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Ubungo, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, jana katika Ukumbi wa CCM manzese jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Janeth Masaburi (kushoto) akisebeneka na baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Manzese wakati wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, jana.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akizungumza na Wenyeviti, Makatibu na Wenezi wa Kata, Makatibu wa Jumuiya ya ngazi za Kata, Wenyeviti wa Mitaa na Mabalozi wa Jimbo la Kibamba, wakati akiwa katika ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Dar es Salaam, katika Ukumbi wa Hoja Kata ya Salanga, jijini Dar es Salaam, jana.
Baadhi ya Viongozi wa Kata ya Salanga Jimbo la Kibamba, wakiwa bize kutunza kumbukumbu ya elimu iliyokuwa ikitolewa kwao na Naibu Katibu Mkuu jana.
Baadhi ya wanachama wa CCM Kata ya Salanga wakisimama na kuimba kumpongeza Naibu Katibu Mkuu wakati wa ziara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo, akiteta jambo na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Kata ya Salanga, Euzedius Chilipwei, wakati akiwa katika ziarayake ya kuimarisha Chama Jimbo la KIbamba jana.
Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Rodrick Mpogolo, akijumuika na viongozi na wanachama wa CCM kufurahi kwa pamoja kucheza muziki baada ya kumaliza kuwahutubia katika ziara yake ya kuimarisha Chama kwenye Jimbo la Kibamba Kata ya Salanga jana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: