Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuachia madaraka kwa kushindwa kusimamia suala la mchanga wa dhahabu unaosafirishwa kwenye makontena.

Amemtaka waziri huyo kujitathimini na bila kuchukua muda mrefu aachie madaraka kutokana na suala hilo.

Rais Magufuli amesema hayo baada ya kamati iliyokuwa ikichunguza suala la mchanga kwenye makontena kukabidhi ripoti yao.

Kamati hiyo ya wataalamu wa jiolojia na uchambuzi wa kisayansi iliyoundwa Machi 29 mwaka huu, ilichunguza aina ya madini yaliyopo, kiasi na viwango vya ubora.

Akikabidhi ripoti hiyo, Profesa Mruma amesema uchunguzi huo umebaini uwepo wa madini ya kiasi cha kati ya Sh829.4 bilioni mpaka 1.439 Trillion kwa makontena yote 277.

"Licha ya uchunguzi uliofanywa kupitia makontena haya, tumegundua uwepo wa aina nyingi zaidi za madini ambayo hayakuwa yakijulikana na haya yamekutwa na thamani ya kati Sh129.5 bilioni mpaka261 bilioni," amesema Profesa Mruma.
---
 
Huu ni muhtasari wa kamati ya uchunguzi wa mchanga wa madini kama ulivyowasilishwa na mwenyekiti wake Prof Abdulkarim Hamis Mruma hii keo Ikulu!.

HADIDU ZA REJEA!.

1.Kamati ilikuwa na kazi ya kuchunguza aina na kiwango cha madini yaliyopo ndani ya mchanga wa madini unaosafirishwa nje!.

2.Chimbuko la utafiti huo ni kutojulikana kwa kiwango cha makinikia na mikataba yake!.

3. Hadidu za rejea zilikuwa ,Kufanya uchunguzi wa makinikia kwenye bandari ya dsm na migodini,Kufanya uchunguzi wa kimaabara ili kujua thamani na aina ya madini yaliyopo kwenye makilikia,kuchuza uwezo wa scanner zilizopo bandarini,kuchunguza uwezo wa TMAA katika kusimamia makinikia,

4.Kamati ilitembelea bandari ya Dsm,bandari kavu na kwenye migodi ya Bulyanhuru na Buswagi,yapo makontena ambayo kamati ilichukua sampuli ya juu na chini,sampuli nyingine ilikuwa zigzaga!.

5.Kamati ilichunguza uwezo wa scanner kupima makinikia!.

6.Kamati ilikokotoa thamani ya madini yaliyopatikana kwenye makinikia!.

MATOKEO YA UCHUNGUZI

1.Kamati imebaini uwepo wa dhahabu kiasi Kikubwa cha dhahabu kwenye makinikia,katika makontena 277 yaliyozuiliwa kulikuwa na tani saba za dhahabu!.
2.Makontena 277 yaliyozuliwa yalikuwa na dhahabu yenye thamani zaidi ya shilingi Trilioni moja nukta moja nne saba!.

3.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya shaba,Silver,surpher,chuma.

4.Copper pekee ilikuwa ya thamani ya shilingi Bilioni 23.3,hapa kulikuwa na tofauti kubwa na ripotibya serikali ambayo ilionesha kuwa na thamaninya Bilioni 13.

4.Upande wa silver kamati ilibaini uwepo wa silver ya thamani ya bilioni 2.1.tofauti na ripoti ya Serikali ilionesha thamani ya Bilioni 1.

5.Upande wa surpher kamati ilibaini uwepo wa surpher ya thamani ya shilingi bilioni 1.9,kamati ilibaini madini madini haya hayapo katika mrabaha

6.Kamati ilibaini uwepo wa madini ya chuma yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.3,

7.Kamati ilibaini uwepo wa madini mkakati ambayo kwa sasa yanahitajika sana duniani yenye thamani kati ya bilioni 129.5 mpaka bilioni 261.5

Thamani ya madini yote katika makinikia kwenye makontena 277 yaliyochunguzwa kamati imebaini yana thamani ya triloni 1.339,ambazo serikali haipati hasa senti moja na hayapo kwenye mrabaha!.

8.Kamati imegundua uwepo wa madini mengine mengii ambayo hayarekodiwi kwenye nyaraka za serikali!.

9.Kamati imebaini wakala wa madini Tanzania hawafungi utepe kwenye makontena kuonesha viwango vya madini,kamati imebaini ufungwaji huu kufanyika wakati wa kusafirisha makontena.

10.Kamati imebaini scanner za bandarini kutokuwa na uwepo wa kubaini utotoshwaji wa mali!.

MAPENDEKEZO YA KAMATI

1.Serikali isitishe usafirishaji wa mchanga nje ya nchi

2.Serikali ihakikishe mitambo ya kusafisha makinikia unafanyika nchini

3.TMAA ifunge utepe mara baada ya mchanga kupakiwa kwenye makontena!.

4.TMAA ipime metal zote kwenye makininia

5.TMAA ipime viwango vyote vya makinikia na madini kwenye mbar bila kujali ripoti ya msafirishaji hii itasaidia Serikali kupata mrabaha!.

6.Serikali iwachukulie hatua watendaji wa TMAA na wizara husika.

7.Serikali iweke mfumo kushtukiza kwenye udhibiti wa madini!.

8.Serikali itumie wataalam wa mionzi kwenye scanner za bandarini!.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: