Monday, May 29, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AMTEUA SIMON SIRRO KUWA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA (IGP)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzabia Dkt. John Magufuli, amemteua kamishina wa polisi Simon Sirro kuwa mkuu wa jeshi la polisi (IGP).

Kabla ya uteuzi huo IGP Simon Siro alikuwa kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam.

IGP Simon Sirro anachukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa iliyotolewa na katibu mkuu kiongozi balozi John Kijazi imeeleza kuwa IGP Simon Sirro ataapishwa kesho Jumatatu katika Ikulu ya jijini Dar es Salaam.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu