Tuesday, May 16, 2017

WADAU WAKUTANA KUJADILI UDHIBITI WA BIASHARA HARAMU YA BINADAMU

Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya kuzuia biashara hiyo. Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu. Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya kupambana na biashara hiyo, ambaye pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating. Mafunzo hayo yanashirikisha wadau mbalimbali kutoka katika nchi zilizopo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mratibu wa Mradi wa Shirika la Wahamiaji la Kimataifa nchini, Tamara Keating, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,Wengine ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu,ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere na Afisa Mkuu wa Kitengo cha Jinsia kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Dk. Joseph Pitso . Mafunzo yanashirikisha wajumbe kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Binaadamu, Separatus Fella, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu yanayoshirikisha nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC). Mafunzo hayo yanafanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mtoa mada kutoka nchini Zimbabwe, Jacinta Hofnie, akiwasilisha mada kwa washiriki wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu kutoka katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayofanyika jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binaadamu, ambae pia ni Mgeni Rasmi, Adatus Magere (watatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Mafunzo ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu katika nchi zilizomo katika Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) yanayofanyika jijini Dar es Salaam.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu