Monday, May 29, 2017

WASANII WANOGESHA UZINDUZI WA TAMASHA LA GULIO LA MTAA LA KITUO CHA REDIO 102.5 LAKE FM

Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni akiwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza katika kampeni hiyo na kuwaomba kuitumia kituo chao kupaza sauti.
Wafanyakazi wa kituo cha 102.5 Lake FM wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mama Ntilie waliopewa mafunzo ya upishi wenye usafi wa hali ya juu na kuzawadiwa zawadi mbalimbali wakati wa tamasha la Gulio la Mtaa.
Mwakilishi wa kampuni ya Tigo, Baraka Siwa akizungumza katika tamasha hilo.
Msanii ajulikanaye kwa jina la Manota kutoka kikundi cha Tanzania Youth Talent (TYT) akionyesha manjonjo katika uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM ya Mwanza.
Msanii wa hip hop, Abuu Mkali akifanya onyesho atika tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.
Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili wa kikundi cha Thimba wakifanya onyesho lake kwenye tamasha la Gulio lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.
Msanii nyota wa muziki wa hip hop wa Mwanza, Kembo akifanya onyesho kwenye tamasha la Gulio lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM kwenye mnada wa National, Nyakato mkoani Mwanza.
Umati wa watu uliofika katika uzinduzi wa tamasha la Gulio la Mtaa lililoandaliwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM ambalo lilifana sana.

Zaidi ya wasanii 20 wa muziki wa hip hop, bongo fleva, zouk, taarabu na ngoma za asili wa Kanda ya Ziwa walinogesha uzinduzi wa kampeni ya Gulio la Mtaa iliyoanzishwa na kituo cha redio cha 102.5 Lake FM katika mnada wa wafanya biashara wa National, Nyakato wilaya ya Ilemela mjini Mwanza.

Wasanii hao ni Dogo D, Ngeta, H Mkali, G Stanza, Goliath, D Chance ambao ni wa hip hop wakati wa bongo fleva ni Abuu Mkali, King Suva, l Mavoko, Sania, na Lakezonia wakati wa zouk ni Sanja, Man Je Paul na Pradetha.

Mbali ya wasanii hao, pia kulikuwa na msanii wa taarabu, Fatina huku kwa upande wa ngoma za asili kulikuwa na Kanyau, Shimba na KG wakati kwa upande wa muziki wa Raga alikuwa myota wa miondoka hiyo Volcano.

Tamasha hilo pia hakikuwa sahau wasanii wa vichekesho kama Mama Manungwa, Malale na Mayala huku kikundi cha Tanzania Youths Talent (THT) kikionyesha staili mbalimbali za muziki na msanii wa wa wafanyabiashara wa Mnadani, Kembo akionyesha ujuzi wake katika miondoko ya hip hop.

Mbali ya kupata uelewa wa masuala ya biashara, wafanyabiashara hao walipata burudani kutoka wasanii hao nyota kutoka kanda ya ziwa chini ya udhamini wa kampuni ya Tigo, Pepsi, Genic Studios, Lake Zone tents, Busybees Enterprises, Mama Sarakikya decoration na Mamba Entertainment.

Tamasha hilo pia lilishuhudia redio hiyo kwa kushirikiana na wadhamini waliwazawadia Mariam Magembe kuwa mama lishe bora huku Khatibu Ramadhani alishinda taji la mwanazengo hodari.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya biashara ndogondogo, minada na masoko, Justine Sagala, amekipongeza kituo cha 102.5 Lake FM kwa ujio huo kwani amesema ni wazo lenye tija baina ya radio nawananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa 102.5 Lake FM, Doreen Noni aliwapongeza wafanyabiashara waliojitokeza katika kampeni hiyo na kuwaomba kuitumia kituo chao kupaza sauti zao.

“Nimefuraishwa na mwitikio wenu katika uzinduzi huu na hii ni fursa kwenu kujua nini tunachokifanya kwa ajili ya ustawi wa jiji na wananzego kwa ujumla,” alisema Doreen.

Mkuu wa Maudhui na vipindi wa redio hiyo, Yusuph Magupa aliwashukuru mashabiki wote waliofika katika uzinduzi huo na kuwaomba kushirikiana nao.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu