Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga,Yusuf Manji amethibitisha rasmi kujiuzulu wadhifa wake.Katika barua yake iliyopatikana leo Mei 27, 2017 imesema,

“Muda wangu wa kutangaza kuwa ninakaa pembeni kutoka kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Yanga ni sasa.” Alisema na kuongeza tayari tumekuwa mabingwa wa mashindano tena, tuna kikosi cha wachezaji na makocha, tumeungana kwa umoja haijawahi kutokea. 

Tumerudisha heshima ya kuwa washindani wa ukweli katika vilabu vya Afrika na kuwa imara zaidi kiuchumi na mkataba wa ufadhili wa Sports Pesa n.k. Nafahamu kuwa bado kuna mengi yanahitajika kutimizwa, lakini barabara ya mambo yanayotakiwa kutimizwa haizwezi kuisha, na siwezi kuwa mroho kwa kuamini kuwa ni mimi pekee nitaweza kuifikisha mwisho wa safari Klabu yetu.” Alibainisha Manji katika barua yake ya kurasa mbili aliyoisani Mei 22, 2017.

Kupitia taarifa hii, kutoka Mei 20, 2017 mimi Yusuf Mehbub Manji nimeachia ngazi kama Mwenyekiti wa Young Africans Sports Club na Makamu Mwenyekiti wa wangu ndiye ataongoza Klabu hadi hapo patakapofanyika uchaguzi kujaza nafasi ya Mwenyekiti. Alisema Manji katika taarifa yake
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: