Monday, June 12, 2017

AIRTEL NA DTBi WATOA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WALIMU WA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Kompyuta wa Sekondari ya Loyola, Sista Maria Sany, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, katika Shule ya Msingi Kijitonyama jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Magdalena Mtei, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Hisabati na Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Wilfred Ringo, baada ya kuhitimu Mafunzo ya Walimu katika fani ya sayansi kwa kutumia programu za kompyuta ili kuwawezesha kufundisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, yaliyofadhiliwa na Airtel Tanzania na kuwezeshwa na Kituo cha Elimu cha Galway cha Ireland, yaliyofanyika shuleni hapo, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni Meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa nne kulia), Mkurugenzi wa Galway, Bernard Kirk (wa pili kulia) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Beatus Amri.
---
Airtel kuanzisha mahabara ya Kompyuta kwa wanafunzi na vijana kujifunza na kuvumbua application mbalimbali

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikian na DTBi wametoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni katika matayarisho yakufungua maabara ya kompyuta yanayotegemea kuzinduliwa mwezi huu

Mafunzo hayo yametolewa na walimu 6 toka katika Kituo cha Elimu cha Galway nchini Ireland kwa lengo la kuwapatia uwezo , mbinu na maarifa ya technoologia ya kompyuta ili kuweza kuwafundisha wanafunzi watakaojiunga na kutembelea maabara hiyo ujuzi utakaowawezeshaa kutengeneza program ndogo ndogo na baadaye kuweza kuvumbua program kubwa zenye kuleta suluhisho kwa mahitaji mbalimbali ya biashara na jamii

Maabara ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza masomo ya Tehama kuongeza ujuzi, na kutoa mwanga kwa vijana kuwa wabunifu kwa kuzindua application mbalimbali ambazo zitaweza kuwaingizia kipato

Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula alisema “ kutokana na changamoto iliyopo kwa sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza wanapoingia katika elimu ya chuo kikuu kumefanya kuwe na ufinyu katika ubunifu na kutumia technologia katika ujasiriamali. Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwaya kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri mdogo

Mafunzo haya kwa walimu tunayotoa leo ni uthibitisho wa dhamira yetu katika kuhakikisha tunakuwa na walimu bora watakaowasaidia wanafunzi kujikita kwenye technologia na kuwa wabunifu. Aliongeza Mulamula

Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “ tumejipanga kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao kwa kuanzisha maabara hii yenye kompyuta za kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kujifunza mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kutanua wigo wao”

kupitia program ya Airtel Fursa tunayo application ya VSOMO iliyotengenezwa na kjana wakitanzania ambao leo hii inawawezesha maelfu ya watanzania kuipakuwa na kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao za mkononi. Tunaamini maabara hii itakuvumbua na kukuza zipaji vingi na kuleta uvumbuzi katika Tehama. Aliongeza Bayumi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu