Mhe. Balozi George Kahema Madafa katika tukio la kukabidhi hati za utambulisho kwa Rais Wa Jamhuri ya Italia Mh. Sergio Mattarella kwenye Ikulu ya Rais jijini Roma hapo tarehe 18.05.2017. Mh. Balozi Madafa aliambatana na maafisa wawili wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na mkewe Bi. Esther Bhoke Madafa.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Kahema Madafa akapeana mikono na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Kahema Madafa katika mazungumzo na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella na maofisa wake baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma.
Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. George Kahema Madafa akiagana na Rais wa Italia Mh. Sergio Mattarella baada ya kukabidhi hati zake za utambulisho katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Roma. 

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: