Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, akizungumza na Wanachama wa CCM na Viongozi wa UWT, wakati wa ziara ya wabunge hao katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa Jumuiya hiyo na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
Wanachama wakifurahia na kushangilia
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonah Kaluwa, akizungumza kutoa baadhi ya kero za wapiga kura wake mbele ya mgeni rasmi Kiongozi wa Wabunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Dar es Salaam, na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela kairuki, wakati wa ziara ya wabunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dar es Salaam, katika Jimbo la Segerea Wilaya ya Ilala kuhamasisha wanachama kuhusu uchaguzi wa UWT na Uhai wa Chama katika mkutano uliofanyika leo mchana kwenye Ukumbi wa CCM Liwiti Tabata Dar es Salaam.
---
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, kimesema kitapambana kufa na kupona kuhakikisha majimbo sita yaliyochukuliwa na upinzani yanarudi mikononi mwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

Aidha wabunge hao wamewataka viongozi waUmoja wa Wanawake CCM (UWT) waliopoteza majimbo kutopewa tena nafasi katika chaguzi zinazoendelea kwa maslahi ya uhai wa Chama.

Akizungumza jana Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki akiongoza ziara ya wabunge hao wilaya ya Kinondoni alisema hakuna haja ya kumuonea mtu haya lengo ni kuhakikisha majimbo hayo yanarudi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Alisema ni muhimu kila mmoja kabla ya kuwania nafasi ya uongozi ndani ya UWT kujipima na kujitafakari uwezo wake kama ana kifua cha kukihakikishia chama kinarejesha majimbo hayo.

‘’Tutahakikisha CCM Mkoa wa Dar es Salaam tunapambana kufa na kupona kurudisha majimbo sita yaliyochukuliwa na upinzani yanarudi mikononi mwetu hakuna muda wa kusubiri tukikosea katika chaguzi za ndani tumekosea baadae kushawishi na kurejesha uhai wa chama,’’alisema.

Alisema ni lazima kuingia katika chaguzi hizo kwa kujitafakari na kutochukua fomu kwa waliosababisha kupoteza majimbo hayo kutokana na kutojipanga kwao.

Angellah alisema ni jambo la ajabu na aibu wanawake kukubali kupoteza majimbo hayo kwa kushindwa kujipanga na kuhamasishana kujiandikisha kupiga kura.

Alisema wakati wa kujutia makosa ni sasa hivyo Jumuiya hiyo ikiwa inaendelea na chaguzi zake ni muhimu wanachama wahakikishe hakuna kuchaguana maswahiba ‘maboya’ na badala yake wachague mtu kwa sifa yake ili aweze kuchapa kazi kwa umakini zaidi.

Alisema Kinondoni idadi ya watu waliochukua fomu ukilinganisha na wanachama waliopo ni ndogo hali inayotishia kuwapo na hujuma hivyo ni lazima kujipanga lengo si kuwa kiongozi kwa mazoea kwakuwa chama si mali ya mtu mmoja.

‘’Ni aibu haiwezekani nafasi moja mtu mmoja au wawili na yupo yeye na swahiba yake au boya lake haiwezekani ni lazima kuwa makini hayo maboya mliyoweka yanaweza kuja kuibuka na matokeo yake chama kikakosa nguvu ya kupambana kurejesha majimbo hayo,’’alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo utendaji hautakuwa na sifa stahiki bali utakuwa wa kuogopana na hakutakuwa wa kumkanya mwenzake.

Angellah alisema baada ya uchaguzi huo anaamini kuwa makundi hayatakosekana lakini ni vyema kubaki na mtu ambaye ameshinda na wote kumuunga mkono.

Pia alishitushwa na idadi ndogo ya vijana ambao wanaingia katika chaguzi hizo huku akiwataka wasinyimwe nafasi kwa maana vijana ndio taifa la leo na kesho.

Waziri Kairuki pia alibainisha kuwapo na harufu ya ufisadi katika kata ya Ndugumbi Wilaya ya Kinondoni kutokana na matumizi mabaya ya mali za UWT zikiwemo fedha na vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya wanawake kujitafutia kipato.

Alisema hayo yamesababishwa na kutokuwa na viongozi madhubuti wa kusimamia mali za chama.

‘’Tulipochaguliwa tulirudi kuwashukuru na tulitoa mashine tatu za kusaga na tatu za kukoboa, Vyerahani Saba lakini huu ni mwaka wa sita vinaozea Wilayani na vingine mtu kajimilikisha anatumia kama vya kwake binafsi ni lazima sasa kuanza kufuatilia mali za UWT na kurejesha kwa wanachama,’’alisema.

Aliongeza mbali na vifaa hivyo pia zilitolewa mashine za kutotoreshea vifaranga na fedha za kodi kwa kila jimbo ni lazima zirudi na kuelekezwa kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam Fatuma Maliyaga aliwataka wanachama wa Jumuiya hiyo kuachana na dhana potofu wanaposhindwa chaguzi kwa kuwa na makundi na badala yake washirikiane kwa maslahi ya Chama.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: