Thursday, June 29, 2017

DALILI 10 ZA KUCHOKWA NA MPENZI WAKO, KAMA ZIPO MBILI TU, ACHIA NGAZI MCHUMA UONDOKE

1. Hupigiwi simu hadi umpigie.

2. Hutumiwi sms hadi umtumie.

3. Usipomtafuta halalamiki wala hakuulizi.

4. Ukimpigia simu muongee muda mrefu kidogo anakwambia yupo busy daily.

5. Ukimpigia simu usiku anakwambia anataka kulala au simu haina chaji, lakini ukikaa kidogo ukipiga tena unakuta inatumika au unamuona online.

6. Kama upo naye group, anaamkia kwenye group kusalimia watu na akifanya hivyo anaamini hata wewe amekusalimia.

7. Ukituma texts hata awe online haisomi na akiisoma kujibu ni OPTIONAL COURSE.

8. Ukichat naye anakupa majibu mafupi kama short course za computers studies.

9. Hajawahi kukuweka DP hata siku moja, ingawa wewe ungependa afanye hivyo. Kisingizio chake eti baba na mama yake wapo watsap ingawa kwa ukubwa na tabia zake hata wazazi wake wanajua kuwa ana wapenzi (sio mpenzi).

10. Kukutambulisha kwa watu ni mbinde, na anatabia za kuwasifia rafiki zako kuliko huku wewe maneno yenye ladha ya mapenzi yakikujia usingizini tu.

Mwanaume au mwanamke mwenye tabia hizi hafai kuwa mpenzi wako mkimbie kama ukoma.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu