WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akicheza sebene na muongoza shughuli 'Mc' Mussa , wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama.
RAPA Mwanamke Ruth Nzele, wa mwanamuziki wa Kimataifa kutoka Congo, Ferre Gola, akirap wakati bendi yake ikitoa burudani katika onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017. 
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akipiga makofi kumshangilia mnenguaji wa Ferre Gola, Ilunga Mulumba, wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017.
Mnenguaji wa Mwanamuziki Ferre Gola wa Congo, Ilunga Mulumba, akipagawisha mashabiki wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017.
Mnenguaji wa Mwanamuziki Ferre Gola wa Congo, Biffalo Yamado, akipagawisha mashabiki wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia leo Juni 30, 2017.
Mwanamuziki Ferre Gola wa Congo, Djany Pacha, akiwa hewani baada ya kubinjuka sarakasi wakati wa onesho maalumu la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia jana Juni 30, 2017.
WAZIRI wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga, akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga, kwa kutambua mchango kufanikisha onyesho la mwanamuziki Ferre Gola, la kusherehekea Uhuru wa miaka 57 ya Nchi ya Congo lililofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia jana Juni 30, 2017. Fedha zilizopatikana kutokana na mauzo ya meza za onyesho hilo zinasaidia kuchangia Wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule za Uhuru Mchanganyiko na Wama. Kulia ni Balozi wa Congo nchini Tanzania, Jean-Pierre Mutamba (kushoto) ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Ltd, na mratibu wa onyesho hilo, Teddy Mapunda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: