Kiroba cha mchele kikishushwa kwenye gari la Global Tv Online waliotoa msaada huo kwenye Kituo cha Kulelea Yatima, Umra, kilichopo Magomeni, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi kesho.
 
Mlezi wa kituo hicho, Rahma Kishumba akitoa shukrani kwa Global Tv online baada ya kupokea zawadi hizo ya iddi. 
Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo, kulia akimkabidhi mlezi wa kituo hicho, zawadi hizo. ...sehemu ya zawadi hizo.
 
Watoto wakionesha tabasamu baada ya kuona zawadi zao.
Mlezi wa kituo hicho akitoa shukrani zake kwa Global TV huku akicheka kwa furaha[/caption]
Mtoto Rahma Yusuf (6) akiishukuru Global Tv kwa niaba yab watoto wenzake baada ya kukabidhiwa zawadi.
Watoto wakiwa na zawadi zao baada ya kukabidhiwa.
Global Tv Online inayomilikiwa na Kampuni ya Global Publishers, leo imetoa msaada wa vitu mbalimbali kikiwemo chakula, vinywaji na sababu kwa watoto yatima wa Kituo cha Umra kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alikabidhi mchele, unga na sukari pamoja na vinywaji mbalimbali pia sabuni kwa ajili ya sikukuu ya Iddi inayotarajiwa kusherehekewa kesho na aliwatakia sikukuu njema watoto hao.

(PICHA; RICHARD BUKOS/GPL)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: