Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shda la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya ajali ya ndege ya kivita iliyotokea mwaka 1978 kwenye Msitu wa Muhunda, wilayani Butiama mkoani Mara. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Mama Maria Nyerere nyumbani kwa Mama Maria Butiama leo mara baada ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipanda mti kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa imeadhimishwa Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwagia maji mti alioupanda kwenye Msitu wa asili ulioasisiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kitaifa meadhimishwa Butiama.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akiwahutubia Wananchi kijijini Butiama mkoani Mara wakati wa kilele cha siku ya mazingira Duniani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kiatu cha kusaidia walemavu wakati alipotembelea banda la Kituo cha Walemavu cha Ziwa Victoria (Lake Victoria Disability Centre) kinachoshughulika na kutengeneza viungo bandia kwa watu wenye ulemavu kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge, Butiama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia namna samaki anaweza kufugwa vizuri bila kuharibu mazingira na kuleta manufaa kabla ya kuhutubia kwenye kilele cha siku ya mazingira duniani ambapo kilele chake kimefanyika kwenye viwanja vya Mwenge, Butiama.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kwa viwanda na migodi
ambayo inafanya shughuli zake za uzalishaji kwa kuharibu mazingira ikiwemo utitirishaji wa kemikali kwa wananchi kwani kufanya hivyo
kunahatarisha usalama wa wananchi na viumbe hai wengine.

Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo tarehe 4-Jun-2017 kijijini Butiama mkoani Mara wakati anahutubia wananchi katika kilele
cha siku ya mazingira Duniani.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema uharibifu wa mazingira ukiachiwa uendee nchini ni hatari kwa usalama wa maisha na viumbe hivyo ni muhimu kwa viongozi katika ngazi zote kuchukua hatua zitakazosaidia kukabiliana na vitendo hivyo
kote nchini.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa umefika wakati kwa viongozi kwa ushirikiano na jamii kuhakikisha wanaweka mikakati ya kuokoa mifumo ya ikolojia, uhifadhi wa bioanuai, kudhibiti uchomaji miti kiholela ili kurejesha uoto wa asili ambao umeharibiwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu katika maeneo mengi nchini.

“Kutozingatia hifadhi ya mazingira kunaweza kusababisha kuparaganyika kwa mfumo huo na kufanya maisha yetu na ya vizazi vijavyo kuwa mashakani”. Amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema katika kuadhimisha siku ya mazingira Dunia viongozi wanapaswa kuchukua hatua za kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili kila mtu ashiriki katika juhudi za kuwa na uchumi unaozingatia hifadhi ya mazingira.

Kuhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa nchini, Makamu wa Rais aipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuruhusu wananchi kutembelea hifadhi za taifa bila kiingilio na kusema mpango huo ni mzuri na unatakiwa kufanyika kila mwaka.

Amesema kuwa mkakati huo unalenga kuhamasisha wananchi ili kuwa mahusiano rafiki na mazingira kwa kuzingatia ukweli kwamba jinsi wananchi wanapoona ndipo wanapoamini na kuelewa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: