Saturday, June 10, 2017

HUWEZI KUJIITA MWANAUME

Huwezi kujiita mwanaume kama hujui wanao wanakula nini? Huwezi kujiita mwanaume kama hujui kama nguo walizovaa wanao pesa imetoka wapi? Huwezi kujiita mwanaume kama hujui nguo aliyovaa mkeo, nywele alizosuka na kila kitu chake kimetoka wapi?

Mkeo kufanya kazi sio tiketi ya wewe kugeuka kuwa mwanaume suruali? Kuna watu wengine hujisahau eti kisa mke anafanya kazi basi unafurahia kula kuku kila siku. Hata hujiongezi ukatoa matumizi ya ndani?

Ungekuwa na akili kidogo ungejua kuwa mshahara wa mkeo hautoshi kufanya vyote hivyo anavyofanya na ungekuwa makini, sasa wewe unaridhika tu kwakuwa anafanya kazi unamuachia kazi ya kuwa mwanaume.

Nikuambia tu kitu kimoja mwanamke hata awe na pesa vipi bado anahitaji mwanaume wa kumtunza, yaani mtu wa kwenda kumlalamikia shida zake na kumsikiliza. Sio kwenda kulalamikia shida zake kwenye ATM.

Katika familia mwanaume unatakiwa kutoa na mke kuchangia kwamba, hata kama ana kipato kikubwa lakini usibweteke na kumuachia kila kitu, asipoweza kulalamika kwako atatafuta sehemu ya kulalamikia.

Mwanamke anatakiwa kuongezea kilichopungua na si kutoa kisichokuepo. Kwamba mke ni msaidizi, lakini unapomfanya mke kuwa ndiyo mtoaji mkuu basi huna haki yakusema nimeoa bali umeolewa.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu