Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akizungumza na Watendaji na viongozi wa jumuiya hiyo wa ngazi za Mikoa na Wilaya mara baada ya kuwakabidhi komputa.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Zanzibar, Nagma Giga akimkabidhi komputa Katibu wa Wazazi Mkoa wa Kaskazini Bi.Zaituni Bushiri Ussi.
Baadhi ya Komputa zilizokabidhiwa kwa Makatibu wa Mikoa na Wilaya jumuiya ya Wazazi za Zanzibar.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

JUMUIYA ya Wazazi ya CCM Zanzibar imewataka watendaji wake wa ngazi mbali mbali za jumuiya hiyo kuwa waadilifu wakati wa kuchuja majina ya wagombea wanaowania nafasi mbali mbali za uongozi kupitia uchaguzi unaoendelea ndani ya chama na jumuiya zake.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Bi. Nagma Giga wakati akikabidhi vitendea kazi ambavyo ni komputa na printer kwa Mikoa na Wilaya nane za jumuiya hiyo huko katika Afisi Kuu ya Wazazi Mpirani Kikwajuni Unguja.

Alisema watendaji wa ngazi za mikoa na wilaya za jumuiya hiyo ndio wasimamizi wakuu wa uchaguzi huo kwa ngazi mbali mbali za jumuiya hivyo wakati wa kuchuja wagombea ni lazima waweke kando urafiki na undugu na wawapitishe viongozi wenye sifa na uzalendo wa kukisaidia chama kushinda katika uchaguzi mkuu ujao.

“Mafanikio tuliyonayo ndani ya jumuiya yrtu yanatokana na juhudi zenu za kiutendaji hivyo nakupongezeni sana na muendelee na kasi hiyo hiyo hadi tupate viongozi imara watakaotetea maslahi ya CCM mwaka 2020”, alisema Giga.

Aidha aliwasisitiza viongozi hao kuhakikisha wanatunza vizuri vifaa walivyopewa na kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili kurahisisha shughuli za kiutendaji za jumuiya.

Akitoa neno la shukrani Katibu wa Wazazi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Bi. Zaituni Bushiri Ussi aliahidi kuwa vifaa hivyo vitakuwa ni chachu ya kuharakisha maendeleo ya taasisi katika harakati za kiutendaji.

Naibu Katibu Mkuu huyo ametoa Komputa nane zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa Mikoa na Wilaya zote za Jumuiya hiyo Zanzibar ili kukamilisha ahadi alizotoa katika ziara zake visiwani humo.

Komputa hizo zimetolewa kwa Mkoa Kaskazini Unguja, Mkoa wa Kusini Unguja, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkoa wa Kusini Pemba, Wilaya ya Kaskazini “A”, Wilaya ya Dimani, Wilaya ya Amani na Wilaya ya Amani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: