Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akizungumza na wanahabari wakati wa kutoa zawadi kwa watoto Yatima wa Kituo cha Mtoto Wetu Tanzania jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Miradi wa Kampuni hiyo, Gasparino Haule akiongoza kucheza katika hafla hiyo.
Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni hiyo, Grace Zikwaze, akizungumza na watoto hao.
Keki maalumu ya hafla hiyo ikikatwa kwa pamoja. Kushoto ni Makamu Mkurugenzi wa Kituo hicho, Theobald Truphone na katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo. Wengine ni maofisa wa Kampuni ya Trumark.
Zawadi zikitolewa.
Mwanafunzi Wanswekula Zacharia akizungumza na wanahabari kuhusu changamoto walizonazo.
Nguo zikiandaliwa tayari kukabidhiwa watoto hao.
Keki maalumu kwa ajili hayo iliyotolewa na Kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akiwalisha keki watoto hao.
Picha ya pamoja kabla ya kuicharanga keki hiyo tayari kwa kuila.

Na Dotto Mwaibale.

JAMII imetakiwa kujenga moyo wa kusaidia watu waliopo katika makundi yenye uhitaji ili nao wajisikie kama watu wengine waliopo katika familia.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark inayojishughulisha na uwezeshaji jamii, Agnes Mgongo wakati kampuni hiyo ilipokuwa ikitoa zawadi ya Sikukuu ya Eid El-Fitr katika Kituo cha watoto Yatima cha Mtoto Wetu Tanzania kilichopo Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo hii.

"Ni vizuri jamii ikajenga tabia ya kuwakumbuka watoto na watu wengine waliopo katika makundi maalumu kwa kuwafariji badala ya kuiachia serikali ambayo ina mambo mengi ya kufanya" alisema Mgongo.

Alisema kampuni yake iliguswa na changamoto walizonazo watoto waishio katika kituo hicho ikaona ni vizuri katika kipindi hiki cha sikukuu ya Eid El-Fitr wakajumuike nao kwa kula na kucheza pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: