Tuesday, June 13, 2017

KILIO CHA WANANCHI WA NYAMONGO

 Picha na Maktaba. 
---
Na Amini Mgheni.

Suala la makinikia na maamuzi ya mkuu, yamenikumbusha safari ya Tarime kwa mara ya kwanza ilikuwa wakati wa kampeni zaidi ya miaka saba iliyopita nikiwa Tarime, nilifanikiwa kuwa karibu sana na rafiki yangu ambaye sasa ni Mbunge wa Tarime vijijini John Heche.

Nikiwa kule aliniambia kaka usidhani imetokewa tukawa wapinzani,tumezika sana ndugu zetu kwa sababu ya mapambano ya kutaka madini haya yatunufaishe, ndugu zetu wengi ni walemavu kwa risasi na vipigo kutoka kwa askari wetu waliolipwa na kupewa fedha na kutetea wanyonyaji.

wakati huo John Heche alikuwa amesimama sehemu ambayo aliniambia ''eneo hili kaka nilipiga Magoti na kulia kwa uchungu nikiwa diwani nilichana vifungo vya shati langu nyuma yangu walikuwa wanatarime waliochochwa na dhuluma nilifungua kifua changu na kupaza sauti kuwaambia polisi wanipige risasi tena kifuani''

Nilimsikiliza John Heche aliyekuwa akiongea kwa sauti ya upole lakini yenye ubabe wa kitarime,nilisema kimoyomoyo huyu ni mwanasiasa ngoja niende kwa wananchi nilikuta lugha ya John Heche ndio alivyokuwa kwa wananchi eneo la nyamongo,tulizunguka na kuona milima ya vifusi akaniambia humu ndio makaburi yetu kaka,sijui kama John Heche anakumbuka lakini nakumbuka sana

Nilitoka hapo nikiwa nimelowana na simanzi ya wanyonge,nashukuru baada ya kampeni uchaguzi ulipita,wizara ya nishati na madini ilikumbwa na dhoruba nyingi,wakati huo katibu mkuu aliteuliwa kuwa Eliakimu Maswi akitokea ikulu.

Eliakimu Maswi alifanya kazi kubwa ya haraka (mnyonge mnyongeni haki yake mpeni)alifanya mkutano wa siri baina ya baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari mkutano huo wa ndani ulifanyika Tanga wenye lengo moja tu alisema nimewaitia hapa na watendaji wote wa wizara ya nishati na madini muwaambie madudu yao hapa haalafu wajue kuwa wananchi wanajua uchafu wao wakimaliza hapa wakafanye kazi asiyetaka aniambie.

Tukiwa pale nilikumbuka hadithi ya John Heche kule tarime kwenye vifusi vya madini na sauti za wananchi,wakati huo Kaminshna wa madini alisimama na kuanza kutueleza sheria ya madini alianza na sehemu ya kwanza ya sheria ya madini ambayo inasema madini ni mali ya umma(mali ya wananchi),alipomaliza tu nilinyoosha mkono nilimuambia Kamishna wa madini nikasema ''Mheshimiwa katibu mkuu unatoka Tarime kama sikosei,hivi kweli kamishna wako wa madini anaweza kwenda pale nyamongo akaitisha mkutano wa hadhara akasoma sheria ya madini kuwa madini ni mali ya wananchi ahalafu wananchi wakamshangilia na kufurahi huku wakusuma VX lake kwa kuwa wananufaika nayo? kama hapana kamishna chunguza uhalali wako wa kuwa katika hiyo nafasi''
Picha na Maktaba. 
---
Katibu mkuu Eliakimu Maswi aligeuka akamuelekea kamishna wa madini akasema nataka iwe hivyo vinginevyo tuachie ofisi za watu.

Uwizi wa mali zetu ulikuwa wa makusudi,kamili nimekumbuka hadithi ya kaka yangu John Heche na kilio cha nyamongo kwa dhumuni moja tu kuna watu wamekuwa kafara kwa muda mrefu sana kutetea unyonyaji huu,hata kama hawatatambuliwa kama mashujaa kwangu mimi naona mashujaa,lakini ushujaa mkubwa ni Rais aliyeamua kusema sasa inatosha na kuchukua hatua hii muhimu tusirudi nyuma tupaze sauti kuunga mkono hili na kusimamia mali za wanyonge.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu