Wednesday, June 14, 2017

MAONI YA MSOMAJI; BUNGE LIMEKOSA UZALENDO KWA MTINDO WA NDIOOOO...

Picha na Maktaba.
---
Na Peter Sarungi (The Next Speaker)

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliuliza kwa uchungu "Watanzania ni nani aliye Turogaa???" Alipokuwa akipokea ripoti ya kamati ya madini. Maana ya swali hili ni ili tumjue mchawi wetu na kumtoa katika mazingira yetu. Hili ni swali ambalo kila mtanzania anatakiwa kujihoji na kufikiria ni vipi tumerogwa na ni nani anahusika.

Mimi kwa tafakuru yangu binafsi nimempata mmoja wa aliye turogaa, Tumerogwa na utaratibu wa kupitisha hoja nzito, sheria nyeti na sera zenye kugusa maslahi ya taifa kwa ushabiki na utaratibu wa Ndiooo... ambao umekuwa ni mtindo usiokidhi tija ya maslahi ya taifa.

Bunge letu ndio chanzo kikubwa cha kuhalalisha unyonyaji wote uliofanywa kwenye sekta mbalimbali. Bunge limetumika kupitisha sheria mbovu, sheria za kinyonyaji, sheria za ukandamizaji, sheria zisizo jali maslahi mapana ya taifa.

Ikiwa leo ripoti inadhibitisha ubovu wa sheria na sera za madini zilizo pitishwa miaka kadhaa kwa mbwembwe na makofi mengi kutoka upande mmoja huku upande mwingin e ukipiga kelele za kukataa uharaka wa kupitisha sheria hizo bila mafanikio, ni dhairi kabisa kwamba wabunge tulio watuma kusimamia maslahi ya taifa kwa kodi zetu hawakuwa na uzalendo hata kidogo. Wao ndio chanzo cha madudu yote haya, madudu haya yamekuwepo kwa miaka mingi bungeni kwa hisani ya kulinda chama na serikali bila kutazama maslahi ya taifa kwa miaka mingi ijayo.

Kutokana na ripoti hii, siwezi kuwa na imani na sheria zote zilizopitishwa na upande mmoja wa wabunge wa chama kama sheria ya madini ilivyopitishwa. Sina imani na rasimu ya katiba iliyopitishwa na upande mmoja wa wabunge wa chama tawala, sitakuwa na imani na bajeti itakayo pitishwa na wabunge wa upande mmoja wa chama maana ripoti imedhibitisha kwamba wabunge hao hawana uzalendo kwa nchi na wapo kwaajili ya kulinda maslahi ya chama na viongozi wao wa serikali.

Nashauri Bunge kuondoa utaratibu wa kupiga kura kwa kelele kisha spika kuamua kwa utashi wake binafsi akisaidiwa na masikio pamoja na macho huku na yeye akitokana na chama.
"Nadhani walio sema Ndioo wameshinda"

I WISH I COULD BE A SPEAKER.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu