Saturday, June 3, 2017

MASAUNI AZINDUA MPANGO WA KUWASAIDIA WAKIMBIZI NA NCHI ZINAZOHIFADHI WAKIMBIZI JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari baada ya Kuzindua Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe Kigoma (CCM), Mhandisi Atashasta Nditiye (kushoto), akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Daniel Nsanzugwako pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Kuhudumia Wakimbizi, Harrison Mseke, wakifuatilia Mada inayohusu Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi iliyokuwa inatolewa na Mratibu wa Mpango huo kutoka Idara ya Huduma za Wakimbizi, Dk. John Jingu (hayupo pichani), muda mfupi kabla ya Uzinduzi wa Mpango huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi zake nchini pamoja na Wawakilishi wa Taasisi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamadi Masauni (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Katavi, Tabora, Kagera na Kigoma, watendaji wa serikali na Baadhi ya Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa yanayofanya kazi nchini, wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kuwasaidia Wakimbizi na Nchi zinazohifadhi Wakimbizi (CRRF Tanzania). Uzinduzi huo umefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI –WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu