Katibu Tawala mkoa wa Dodoma, Rehema Dendegu akifungua mafunzo ya siku mbili ya mfumo mpya wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS katika ukumbi wa LAPF Conference Centre Dodoma.
Nyaborogo Patrick Marwa, Mhasibu wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino akichangia wakati wa mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS.
Mkuu wa kitengo cha Mifumo ya Fedha wa Mradi wa PS3, Dkt. Gemini Mtei, akielezea lengo la
mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS wakifanya mafunzo kwa vitendo baada ya maelekezo kutoka kwa wakufunzi.
Mwezeshaji wa mafunzo ya mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS, Abdul Kitula, Mshauri wa Udhibiti wa Fedha za Umma wa mradi wa PS3 akifundisha washiriki namna ya kutumia mfumo huo.  Mroki Mroki wa Daily News-Habarileo Blog.
---
SERIKALI sasa itaanza kupeleka rasilimali fedha moja kwa moja kwenye vituo vya afya kwa ngazi za halmashauri ikiwa ni moja ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Upelekaji wa Rasilimali Fedha moja kwa moja kwa vituo vya kutolea huduma itahakikisha kuwa Fedha zinazotolewa na Serikali zinatumika kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Mkakati huu mpya wa kuboresha sekta ya afya unatekelezwa kwa njia ya msaada kutoka Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), kupitia Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3).

Vituo vya kutolea huduma ambavyo vitapokea fedha hizo vinajumuisha Zahanati, Vituo vya Afya, na
Hospitali za Wilaya. Zoezi hili ni sambamba na inavyotekelezwa kwenye sekta ya elimu, Serikali za Vijiji na Ofisi za Kata.

Mfumo huu mpya wa kupatiwa rasilimali fedha utatoa motisha kwa vituo vya kutolea huduma za afya na kuongeza kipaumbele cha utoaji huduma bora kwa wananchi wa Tanzania na kuongeza usawa na uwazi.

Aidha kupitia mfumo huo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa unaojulikana kwa Kiingereza kama Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS) unasaidia utekelezaji wa utoaji wa rasilimali fedha moja kwa moja kwa ngazi za vituo vya kutolea huduma kwa kuimarisha uhitaji wa kuwepo kwa usimamizi wa fedha katika ngazi ya vituo vya kutolea huduma.
ye uhitaji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: