Sunday, June 4, 2017

MKOLANI VETERANI NDIYO MABINGWA WA 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017' MWANZA

Mkurugenzi wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege (kushoto) akiwa na mgeni Rasmi Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo (katikati) kwa pamoja wakikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa team captain wa Mkolani Veterani Fc mara baada ya kuibuka kuwa Mabingwa wa 'JEMBE FM SPORTS RIPOTI BONANZA 2017, katika uwanja wa Nyamagana. Chini ya udhamini wa Nebrix Limited wauzaji wa vifaa vya michezo na Lake Zone Tents Supply.
Si mchezo 'Miaka miwili ya changamoto hatimaye sasa nuru imeonekana'
Risala ya maadhimisho ilisomwa na Elikana Mathias.
Safu ya Meza kuu.
Mbele ya eneo la kivuli tulilolichagua kuwa jukwaa kuu.
Mkurugeniz wa Jembe Media Group Dr. Sebastian Ndege akitoa shukurani kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza wapenzi wa soka na burudani mara baada ya ushiriki wao kuweza kufanikisha tamasha la kusherehekea miaka miwili ya kipindi cha 'Sports Ripoti' kinachoruka kila siku usiku saa 3 kamili hadi 4 ikiwa ni kwa mara ya kwanza tukio hilo kufanyika, naye ameahidi kwamba maadhimisho hayo yatakuwa yakifanyika kila mwaka ambapo mwakani yataboreshwa zaidi.
Meneja wa Vipindi Redio Jembe Fm Mwanza Timothy Ngalula aka Mbaba Vc sanjari na kutoa shukurani kwa wadau Mwanza na mikoa tofauti tofauti (kupitia Internet) hapa alitambulisha safu ya watangazaji vitengo na vitengo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akihutubia mamia ya wananchi mkoa wa Mwanza waliofika uwanja wa Nyamagana
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji meneja wa kipindi husika Elikana Mathias.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika ambaye pia ni team captein Juma Ayoo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika 'Masamaki'.
Katibu Mkuu wa Chama cha Soka mkoa wa Mwanza, Leonard Malongo ambaye alikuwa Mgeni rasmi wa Maadhimisho ya miaka miwili ya kipindi cha Sports Ripoti cha Jembe Fm akimlisha keki mtangazaji wa kipindi husika 'Sports lady' Vanessa.
Kona ya kushoto upande wa Kaskazini Magharibu...
Wayaaaaaaa kipa wa Mjengoni Fc akiutizama mpira ....ukizama kimiani.
Mkolani Veterani wakisherehekea mara baada ya kuwafungwa kwa penati Mjengoni FC aka Bodaboda kutoka Sauti Malimbe jijini Mwanza.
Nyuma ya kamera.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu