Sunday, June 18, 2017

MKURUGENZI WA HAMIDU CITY PARK, KIGAMBONI AWAANDALIA FUTARI WAISLAMU, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI

Hamidu Mvungi miliki wa kijiji cha Hamidu City Park, Mikwambe Kibada akizungumza na wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari aliyowaandalia wageni wake wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa ambapo aliwashukuru wageni waalikwa hao kwa kujumuika naye katika futari hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan, huku akiwatambulisha makazi hayo yenye nyumba za kuuza ambapo ameshirikiana na mabenki mbalimbali na kukopesha kwa watu wanaohitaji nyumba katika kijiji hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akimshukuru Hamidu Mvungi mara baada ya kushiriki katika futari hiyo pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria.
Mtangazaji wa Chanel Ten na MC wa Shughuli hiyo ya Futari Albert Kilala akikaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa na Mwenyeji wake Hamidu Mvungi wakiongoza wageni waalikwa katika futari hiyo.
 
Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria katika futari hiyo wakichukua chakula.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa katikati, Mwenyeji wake Hamidu Mvungi pamoja na wageni wake wakipata futari.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando pamoja na wageni mbalimbali waalikwa wakishiriki katika futari hiyo iliyoandaliwa na Hamidu Mvungi nyumbano kwake Kigamboni.
Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki katika futari hiyo.
Hamidu Mvungi na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa wakiwa katika picha ya pamoja.
Hamidu Mvungi na mkewe wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni wao.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu