Friday, June 2, 2017

MSHINDI KOMBE LA SPORTPESA KUWAVAA EVERTON DAR JULAI 13, 2017

Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (kushoto) akimfurahia na kumpigia makofi,kijana Abubakar Said wa Kituo cha michezo cha Wakati ujao wakati wa Kliniki iliyofanyika Uwanja wa Taifa, leo. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa pili kushoto) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone (kushoto) Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, wakati wakiwasili Uwanja wa Taifa leo Juni 1, 2017 kwa ajili ya kukagua timu za vijana (Academy) wakati wa zoezi la kuhamasisha vijana katika mchezo wa mpira wa miguu, lililoongozwa na mchezaji huyo wa zamani wa Everton.
Mtoto Hamis Kassim wa Kituo cha michezo cha Bom Bom, akionyesha umahiri wake wa kuchezea mpira wakati wa hafla hiyo ya Kliniki iliyoongozwa na mchezaji wa zamani wa timu ya Everton. Leon Osman.
Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone,akizungumza na waandishi wa habari.
---
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar

KAMPUNI ya SportPesa imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa Uingereza, Everton. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.

Tangazo hilo limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Mkuu wa masoko wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi wa Everton Fc ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na wanahabari. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman,akichezea mpira na vijana.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Yourth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Lenox Musombo, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Symbion cha JK Youth, na timu ya Taifa ya Vijana chini ya Umri wa miaka 17, Serengeti Boys, Zuberi Ada, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman, akisalimiana na mchezaji wa timu ya Kituo cha michezo cha Wakati Ujao Duce, Ezekiel Msuva ambaye ni mdogo wa mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania,Simon Msuva, wakati mchezaji huyo alipowatembelea katika Kliniki yao Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (wa Nne kulia) Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Singo, Mchezaji wa zamani wa timu ya Everton, Leon Osman (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Montage Ltd, Teddy Mapunda, wakipita kukagua timu za vijana za Academy, wakati wa Kliniki ya kuwahamasisha katika mchezo wa Soka katika hafla iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo Juni 1, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, (kushoto) akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Everton Robert Elstone, wakati wa hafla hiyoiliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, leo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu