Thursday, June 22, 2017

MWALIMU COMMERCIAL BANK (MCB) YAFANYA MKUTANO WAKE WA KWANZA WA WANAHISA

Afisa Mtednaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo
Mkuu wa kitengo cha Hazina MCB, Nunu R. Saghal (kushoto), akijadiliana jambo na Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki hiyo, Selemani Kijori.
Ambrose Mshula mjumbe wa bodi ya wakurugenzi MCB, (aliyesimama), akizungumza kwenye mkutano huo. Wengien kutoka kushoto, ni Mshauri wa ksiheria wa benki, Upendo Ngaponda, Afisa Mtendaji Mkuu wa MCB, Ronald Manongi, Mkurugenzi wa bodi ya benki, Said Kambi, Mwenyekiti wabodi ya wakurugenzi, Herman Kessy, George Fumbuka mwangalizi wa hisa na Mkurugenzi wa kampuni ya kimataifa ya ukaguzi wa mahesabu Ernst&Young, Deokan Mkenda
Mshauri wa kisheria wa MCB, Upendo Ngaponda akizungumzia.
Maafisa wa juu wa benki ya MCB, kutoka kushoto, Charles Shedrack, Frederick Rwabukambara, Valence Lutenganya, na Selemani Kijori, wakijadiliana jambo.
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa.
Wajumbe wakichukua makabrasha tayari kwa mkutano
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano na wengine wakipitia taarifa mbalimbali.
Wajumbe wakijisajilii.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

BENKI ya Walimu, (Mwalimu Commercial Bank Plc-MCB)), iko mbioni kuanzisha huduma ya uwakala wa benki ambapo itashirikiana na mawakala wa sehemu mbalimbali nchini ili kuhakikisha inafikisha huduma za kibenki kwa wananchi wote kwa urahisi, uhakika na unafuu.

Hayo yamesemwa Juni 22, 2017, mkoani Morogoro na Mwneyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya benki hiyo, Bw.Herman Mark Kessy, (pichani), kwenye Mkutano Mkuu wa Kwanza wa Wanahisa wa benki hiyo.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa, benki hiyo pia iko katika mpango wa kutumia huduma za ATM bila ya kadi (Cardless), huduma ambayo itasaidia sana wateja kutumia ATM hata bila ya kuwa na kadi.

“Kupitia huduma hii, wateja wataweza kupata pesa zao kupitia mawakala au kupakua programu maalum kwenye simu zao za kiganjani zitakazowezesha kulipa huduma za maji, umeme pia kutuma pesa kutoka kwenye akaunti zao kwenda kwenye huduma maalum ya benki kwa njia ya simu.” Alifafanua.

Akizungumzia hali ya taasisi za kifedha nchini, Bw.Kessy alisema, MCB iko imara licha ya changamoto zilizojitokeza hivi karibuni kufuatia agizo la serikali kuelekeza taasisi zake zote za serikali na umma kuhamisha na kupeleka fedha zote Benki Kuu na hivyo wateja wakubwa wa serikali walifunga akaunti zao na kuhamishia fedha zao BoT hali iliyosababisha ukwasi mkubwa.

“Lakini sio hilo katika zoezi la serikali la uhakiki wa watumishi wa umma, ilibaini watumishi hewa 19,000 na wakati zoezi hilo likiendelea kwa zaidi ya siku 90 urejeshaji wa makato ulisitishwa, hivyo basi mabenki ikiwemo benki yetu hatukupata marejesho ya mikopo kutoka kwa wafanyakazi walioathiriwa na zoezi hilo na pia kukosa mapato yatokanayo na riba ya mikopo hiyo.” Alisema.

Mwenyekiti huyo wa bodi aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa changamoto nyingine ni sheria inayotaka mabenki ili yaweze kufanya miamala ya fedha za kigeni nje ya nchi zinatakiwa kua na benki washirika ili kupitisha miamala hiyo.

“Kutokana na sheria hiyo, benki za Marekani zimeweka utaratibu mgumu kuhusu ushirikiano na mabenki ya nje, hivyo benki ndogo na za kati zimeshindwa kutimiza masharti ya kupata benki mshirika (Correspondence Banking), kutokana na hilo benki nyingi ndogo na za kati zimepoteza biashara na wateja.” Alifafanua Bw. Kessy.

Hata hivyo Bw. Kessy alisema pamoja na misukosuko hiyo, benki ya MCB imeendelea kufanya vizuri katika kuongeza wateja licha ya kuwa ngeni kwenye soko, ambapo hadi kufikia Juni, 2017 wateja wenye akaunti za akiba wamefikia 28,576 zenye thamani ya shilingi bilioni 5.3 huku idadi ya wateja wa mikopo ikifika 228 wenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 na kwamba benki imeweza kuwafikia wateja katika sehemu mbalimbali za nchi.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu