Monday, June 12, 2017

MWANAMZIKI SAIDA KALOLE AREJEA KWA ARI MPYA NA NGUVU MPYA

Mwanamziki Saida Karoli akizungumza katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya ya O'Rugambo katika futari aliyoandaliwa na wadau wa muziki nchini.
Mwanamziki muziki wa taarabu, Hadija Kopa akizungumza katika uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya ya O'Rugambo katika futari aliyoandaliwa na wadau wa muziki nchini.
Wasanii mbalimbali wakipata futari wakati uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya ya O'Rugambo katika futari aliyoandaliwa na wadau wa muziki nchini iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Wasanii mbalimbali wakipata futari wakati uzinduzi wa video ya wimbo wake mpya ya O'Rugambo katika futari aliyoandaliwa na wadau wa muziki nchini iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu

Mwanamziki Saida Karoli azindua video ya wimbo wake mpya ya O'Rugambo katika futari aliyoandaliwa na wadau wa muziki nchini.

Saida ambaye ni moja kati ya wanamuziki wa mwanzo kuimba kwa kutumia lugha ya asili nchini ambapo alijipatia umaarufu , hasa akitumia luigha ya kihaya kwa sasa anarejea tena kwenye fani hiyo baada ya kupotea kwa zaidi ya miaka sita.

Akizungumzia katika futari hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana Saida alisema kuwa kwa sasa anaona mwanga kwenye muziki kwake kwa kuwa anaona ameanza kufanikiwa kabla hata ya kuanza kuwika sokoni.

Amesema, amekuwa kimya kwa muda mrefu kwa kuwa alikwisha kata tamaa katika muziki na kuwa alikuwa hana imani kama angekuja kuinuka tena lakini kwa sasa amepata uongozi uliorejesha imani yake kwenye tasnia hiyo.

Amesema kuwa wimbo wake wa Maria Salome uliporudiwa na mwanamuziki Nasib Abdul, Diamond Platinumz alipata msukumo zaidi wa kurejea kwenye muziki kwa kuwa hata wanamuziki na mashabiki wa nyimbo zake walionesha shauku ya kumsikia tena.

Saida amesema kuwa kazi zake zitasimamiwa meneja wake mpya, Jonas Albert na uangalizi wa Taasisi ya kukuza vipaji nchini, Tanzania House of Talent (THT), amerejea tena kwenye fani hiyo huku akijihusisha zaidi na nyimbo za asili na kuchanganya na vionjo vya muziki wa Bongo Fleva.

Aliongeza, kwa sasa akiwa chini ya meneja mpya amewezeshwa kuachia wimbo huo wa O'Rugambo ambapo ametoa wimbo na video yake kwa kiwango cha kimataifa.

"Nimerejea ninaomba wanamuziki wenzangu pamoja na wale wote wenye nia ya kuendeleza muziki kunipokea na tushikane mikono ili kazi iende kwa kiwango cha juu zaidi" amesema.

Kwa upande wake Meneja wa msanii huyo, Jonas Albert amesema wimbo wa huo wa O' Rugambo ndio wa kwanza kwa msanii huyo kurejea kwenye chati na anatarajiwa kuachia nyimbo nyingine zaidi.

Amesema, katika wimbo huo ameshirikisha vionjo vya msanii Darasa hasa alipoimba "wacha maneno weka muziki".

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu