Tuesday, June 6, 2017

MWILI WA MAREHEMU DKT. NDESAMBURO WAANGWA KATIKA KANISA LA KKKT KIBOROLONI - MOSHI

Gari lililobeba mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo lilielekea kwenye kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni kwa ajili ya kuombewa. Maziko ya Marehemu Ndesamburo yanafanyika leo nyumbani kwake KDC- Moshi.
Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akiingia kanisani.
Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni.
Viongozi mbali mbali wa Chadema wakiingia katika kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni.
Wabunge wa Chadema wakiwa wamejipanga kupokea mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo katika kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kiboroloni.
Wajukuu wa Marehemu Phillemon Ndesamburo wakielekea kanisani.
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburoukiingizwa kanisani.
Waziri mkuu wa Zamani ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika ibada ya kumuaga aliyekuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
Vingizo wa Chadema wakiwa katika ibada ya kumuombea aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo.
Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburoukiingizwa kanisani tayari kwa maombezi.
Mke wa Marehemu aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Phillemon Ndesamburo (wa pili toka kushoto) akiwa kanisani.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu