Friday, June 9, 2017

PSPF YASAJILI WANAFUNZI ZAIDI YA 250 WA VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM, WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI, (PSS)

Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa,(wapili kulia), na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali za wanavyuo wa elimu ya juu mkoa wa Dar es Salaam, wakionyesha vipeperushi vyenye melezo ya Mfuko huo, baada ya semina ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kuelimisha wanafunzi shughuli mbalimbali za Mfuko na fursa zilizopo. Semina hiyo imefanyika leo Juni 8, 2017.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martn, akifungua semina hiyo leo Juni 8, 2017
Mwenyekiti wa TAHILISO, Bw.Stanslaus Peter Kadugalize,(aliyesimama), akifafanua baadhi ya mambo mwishoni mwa semina hiyo. Wengine kutoka kushoto, ni Katibu Mkuu wa TAHILISO, Bi. Zuhura A. Rashid, Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Neema Lowassa, na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akizunguzma na baadhi ya viongozi wa wanafunzi wa elimu ya juu, walipotembelea kuona jinsi utunzaji taarifa za wanachama wa Mfuko zinavyohifadhiwa. Hii ilikuwa ni sehemu ya semina waliyopewa viongozi hao na maafsia wa PSPF jijini Juni 8, 2017.
---
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

ZAIDI ya wawakilishi 250 wa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kutoka jijini Dar es Salaam wamejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari (PSS), baada ya kushiriki semina ya siku moja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam Juni 8, 2017.

Wanafunzi hao kutoka taasisi 20 za elimu ya juu, wamehudhuria semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na PSPF kwa uratibu wa Taasisi ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania, (TAHILISO), ili kuwapatia elimu wanafunzi hao kuhusu shughuli za Mfuo na faida azipatazo mwanachama ikiwemo mafao mbalimbali.

Kabla ya zoezi hilo la kujiunga na Mfuko, awali Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bi. Costantina Martin, aliwaasa wanafunzi hao kujijengea utamaduni wa kuweka akiba kwani manufaa yake huonekana katika kipindi kifupi.

“Mimi nina mototo yuko chuo kikuu huwa ninampatia fedha kidogo za kujikimu lakini namueleza aweke akiba, ningependa kuwahamasisha vijana mjenge utamaduni wa kujiwekea akiba kidogo kidogo,zile posho mnazopata, na fedha kutoka kwa wazazi wenu, mnaweza kutenga sehemu ya fedha hizo na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima ili kujiwekea akiba.” Alsoema Bi. Costantina Martin, wakati akifungua semina hiyo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu