Thursday, June 1, 2017

PUMZIKA KWA AMANI MZEE WETU MAREHEMU PHILEMON NDESAMBURO

Pumzika kwa amani MZEE wetu marehemu,

MZEE Philemon Ndesamburo,

Hakika ardhi inameza wapendwa wetu.
Nimeumia sana kwa kifo chako ingawa natambua mauti na uzima vi katika bwana.

Natumai umefika katika mikono salama,

Nakuomba msalimie baba yangu mpenzi MZEE Vincent Rimoy.
Kwa jinsi alivyokuwa mkarimu kwa watu wote najua atakua amekupokea kwa furaha na kukukaribisha huko alipo.

Kwa maana yeye ameshakua mwenyeji kwa kitambo sasa.

Kama vile nawaona mmekaa katika vile vikao vyenu vya kunywa kahawa.

Nawaona mkicheka na kufurahi na malaika WA Mungu.

Mwambie wanawe tumemmiss sana, MPE hali halisi ya maisha uliyotuacha nayo huku duniani.

Hakika kifo hakina huruma, kinameza wapendwa wetu.

Pumzika baba yetu MZEE Ndesamburo,
Msalimie baba yangu huko mlipo.

Poleni ndugu zangu Dada Lucy Owenya, Thereza Ndesamburo, Neema Ndesamburo, Sindato, Elia Ndesamburo, kwa kuondokewa na baba yenu mpendwa.

Napenda kuwatia moyo lipo Tumaini katika bwana.
Poleni sana familia kwa ujumla,Mungu mwenyezi awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.

Poleni sana wana Moshi, poleni ndugu wote WA KDC, poleni CDM kanda ya kaskazini, poleni wapenda mabadiliko wote, na taifa kwa ujumla.
Hakika tumempoteza jembe, mpambanaji ni huzuni sana.

Mungu atutie nguvu.

Yeye ndiye aliyetupa na yeye ndiye kachukua,jina lake lihimidiwe. Amina.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu