Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. Katika hotuba yake, Rais Dkt. Magufuli alisema "Mtanzania yoyote mwenye akili timamu ukisikia ripoti kama hii inatia uchungu sana, na ndio maana nashindwa hata niazie wapi?"

Rais Dkt. Magufuli ameamua mapendekezo yote yaliyotolewa yafanyiwe kazi na vyombo husika.
----
MAPENDEKEZO.

Kutokana na uchunguzi kamati imebaini kuna ukiukwaji mkubwa wa mikataba na sheria za madini.

Kamati inapendekeza serikali ifanye yafuatyo:-

1. Serikali kupitia msajili wa makampuni ichukue hatua za makampuni yanaendesha uchimbaji wa madini bila kusajiliwa nchini.

2. Serikali idai mrabaha.

3. Serikali iendelee kuzuia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi.

4. Serikali ianzishe kiwanda cha kuchenja.

5. Serikali ichukue hatua dhidi ya waliohusika ktk uingiaji wa mikataba na kutoa leseni, waliohusika kuondoa.

6. Serikali ifute utaratibu wa kulipa asilimia 90 ya mrahaba na kulipa asilimia 10 baadae.

7.Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa watumishi wa TRA ambao mamlaka ya kodi ishatolea uamuzi.

8. BOT ifuatilie mrahaba wa fedha za kigeni.

9. Serikali ianzishe udhibiti wa viwanja vya ndege vilivyopo katika migodi.

10. Serikali iongeze kiwango cha adhabu kwa makampuni ya madini yanayokiuka mikataba ya madini.

11. Serikali ipitie mikataba yote ya madini na kuondoa misaha yote ya kodi.

12. Sheria iweke kiwango maalumu cha asilimia ya hisa itakayomilikiwa na serikali.

13. Serikali ianzishe wakala wa meli kama ilivyokuwa NASACO.

14. Sheria ya itamke bayana kwamba madini ni maliasili ya watanzania.

15. Sheria itamke mikatana isiwe ya siri.

16. Sheria iweke uwazi na kuondoa mamlaka ya waziri wa nishati na madini.

17. Muombaji wa leseni ya madini aonyeshe atakavyoendesha mafunzo na wataalamu wa ndani.

18. Sheria ielekeze fedha zitokanazo na mauzo ya madini ziwekewe benki ya ndani ya nchi.

19. Serikali ipitie au ifute kabisa sheria ya madini.

20. Serikali igharamie mafunzo kwa watumishi wa serikali ili waelewe kuhusu masuala ya mikataba ya madini.

21. Serikali ifanye kaguzi za mara kwa mara ili kujiridhisha kama kuna kiukwaji za mikataba ya madini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: