Mhe. Seleman Jafo (MB), Akifungua Mkutano wa RBF uliofanyika Jiji Mwanza.
Baadhi ya Washiriki wakifatilia Kikao hicho cha siku moja.
Wajumbe kutoka Mkoa wa Mwanza wakiwa katika kikao hicho.
Washiriki wakiwa katika kikao hicho cha RBF katika kuboresha Vituo vya Afya.
Ilani- Naibu Katibu Mkuu Afya TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula akifafanua Ilani ya Chama Tawala juu yakuboresha huduma za Afya katika kikao hicho.
Baadhi ya Makatibu Tawala wa Mikoa wakiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka TAMISEMI wakiwa katika kikao hicho cha RBF.
Mwakilishi wa World Bank Bibi Gayle Martine akimuelekeza jambo mmoja ya washiriki wa Mkutano huo wa RBF.
---
Serikali imesema haita wavumilia watendaji watakaoshindwa kusimamia ipasavyo mradi wa Malipo kwa Ufanisi katika kuboresha utoaji wa huduma za Afya “Results Based Finance” (RBF) ambao hivi sasa unatekelezwa katika mikoa minane hapa nchini.

Akifungua kikao kinacho wakutanisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Maafisa Mipango kutoka mikoa inayotekeleza mradi wa RBF, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Seleman Jafo, amesema ni lazima kufanyike mabadiliko katika utoaji wa huduma za afya kuleta matokeo tarajiwa.

Naibu Waziri Jafo ametawataka Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri kuhakikisha kuwa utekelezaji wa Mradi wa RBF unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vinavyofanyika kila mwezi ili kuwezesha kujua kiasi cha fedha zilizoletwa kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi huo ili kuweza kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo, ameiomba Benki ya Dunia ambayo ndiyo mfadhili wa mradi wa RBF kuangalia uwezekano wa kuwezesha utekelezaji wa Mradi wa huu kufanyika nchi nzima ili kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini kote.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Dunia Bibi Gayle Martine ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa hatua ambazo inazichukua katika kuhimiza suala zima la uwajibikaji na kusema kuwa hali hiyo imeongeza shauku ya Wadau wa Maendeleo kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na utoaji wa huduma za jamii. 

Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Zainab Chaula amesema ili kufikia malengo chanya yanayotarajiwa katika uboreshaji wa utoaji wa huduma za Afya kila mmoja katika eneo lake inabidi kutengeneza mpango kazi ambao ndio utakuwa dira ya utendaji kazi ili kuleta matokeo chanya.

Mradi wa Malipo kwa Ufanisi katika Kuboresha Huduma za Afya nchini Ulianza mwaka 2015 katika mkoa wa Shinyanga kama eneo la majaribio ambapo hadi hivi sasa unatekelezwa katika mikoa nane ambazo ni Mwanza, Shinyanga, Pwani, Simiyu, Geita, Kigoma, Tabora na Kagera.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: