Thursday, June 1, 2017

SHUWASA YAKUTANA NA WADAU KUJADILI RASMU YA MKATABA WA HUDUMA KWA WATEJA

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro akizungumza katika warsha hiyo.Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA, Deogratius Sulla, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA,Reuben Mwandumbya akielezea umuhimu wa wadau wa maji kujadili rasmu ya mkataba wa huduma kwa wateja
Mwenyekiti wa bodi ya SHUWASA,Deogratius Sulla akizungumza ukumbini
Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga,Agnes Machiya akizungumza.
Afisa Uhusiano wa SHUWASA,Nsianeli Gelard akiendelea kuelezea kuhusu mkataba wa huduma kwa wateja.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii manispaa ya Shinyanga,Hassan Mwendapole akiongoza majadiliano wakati wa warsha hiyo
Warsha inaendelea
Wajumbe wakiwa ukumbini.
Wajumbe wakiwa ukumbini
Wajumbe wakiwa ukumbini.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA) imekutana na wadau wa huduma ya maji kujadili rasmu ya Mkataba wa Huduma Kwa Wateja ambapo mkataba utakaopitishwa na wadau utaanza kutumika kuanzia Julai Mosi, 2017.

Warsha ya kujadili mkataba wa huduma kwa wateja imefanyika leo katika ukumbi wa Vijana Center Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.

Akizungumza katika warsha hiyo, Matiro aliwataka wadau wa maji kujadili rasmu hiyo kwa umakini zaidi ili kuweka mambo ya msingi ambayo yatapunguza malalamiko kutoka wateja ikiwemo ongezeko la bei ya maji kwa watumiaji wa majumbani.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa SHUWASA, Reuben Mwandumbya alisema kutokana mamlaka hiyo kuwajali wateja wake imeona ni vyema kukutana na wadau ili kujadili mkataba mpya wa huduma kwa wateja.

“Mkataba uliokuwepo umemaliza muda wake hivyo tumeleta kwenu rasmu ya mkataba ili tujadili kwa pamoja tuweze kuboresha zaidi huduma ya maji kwa wateja wetu”, alieleza Marco

Miongoni mwa wadau walioshiriki katika warsha hiyo ni meya wa manispaa ya Shinyanga, madiwani, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi mbalimbali, watendaji wa kata, wenyeviti wa serikali za mitaa, waandishi wa habari na wadau mbalimbali.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu