Wednesday, June 21, 2017

TANAPA YAINGIA MKATABA NA TBC KUANZISHA CHANELI MAALUM YA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) kwa pamoja leo wamesaini makubaliano ya kuanzishwa kwa Chaneli maalum ya Utalii itakayohusika na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini kwa soko la ndani na nje ya nchi.

Makubaliano hayo yametiwa saini na Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Devota Mdachi, Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dk. Ayub Rioba na Kaimu Mhifadhi wa NCAA Asangye Bangu.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu