Friday, June 16, 2017

UBA BANK TANZANIA YAINGIZA SOKONI KADI ZAKE MPYA ZA MASTERCARD


Mkuu wa kitengo cha malipo ya kiditali wa bank ya UBA Tanzania, Mr. Priscussy Kessy akiongea na baadhi ya wafanyakazi na wateja wa benki hio wakati wa uzinduzi wa Kadi za Mastercard zitakazoanza kutolewa kwa wateja wa UBA Bank Tanzania.

Mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Tanzania, Mr Peter Makau akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kwa wateja wa bank hiyo ya UBA Tanzania.

Mkurugenzi Mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (kushoto) akikata utepe na mkurugenzi mkuu wa bank ya UBA Mr Peter Makau (kulia) kuashiria uzinduzi wa huduma mpya ya kadi za mastercard kutoka Benki ya UBA Tanzania.

Mkurugenzi mkazi wa Mastercard Tanzania Mr. Anthony Karingi (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa bank ya UBA Tanzania Mr Peter Makau (wa pili kushoto)wakikata keki kuashiria uzinduzi wa huduma hio ya kadi za mastercard ya bank ya UBA Bank uzinduzi uliofanyika leo katika tawi la benki hio lililopo barabara ya Pugu.

Mmoja wa wateja wakubwa wa benki ya UBA Tanzania, Mr Jitendra Kumar Bhardwayi akizungumzia ujio wa mastercard ya UBA Bank ambayo amesema itamsaidia katika kufanya manunuzi kwa njia ya mtandao na kumrahisishia shughuli zake za kibiashara.
Baadhi ya wafanyakazi wa UBA bank Tanzania wakifurahi mara baada ya uzinduzi huo wa kadi za Mastercard za UBA Bank.

Wafanyakazi wa benki ya UBA wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi wa kadi za mastercard kutoka benki ya UBA leo.

Wafanyakazi wa benki ya UBA na baadhi ya wafanyakazi wa Mastercard Tanzania wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya uzinduzi wa Kadi mpya za Mastercard za benki ya UBA Tanzania.

Na Josephat Lukaza - Lukaza Blog
 
Benki ya UBA Tanzania imezindua huduma yake mpya ya kadi za mastercard ambazo zitaanza kutolewa kwa wateja wake nchni Nzima. Wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa kitengo cha digitali za benki hio ya UBA Bank Bw Priscussy Kessy amesema kuletwa kwa kadi hizo za mastercard kwa benki yao itawasaidia wateja wao kufanya manunuzi kwenye tovuti mbalimbali na pia zitatumika pia kutolea pesa katika mashine za kutolea pesa zote duniani zenye nembo ya mastercard iwe ndani ya nchi au nje ya nchi.

Uzinduzi huo uliohudhuriwa na wafanyakazi wa UBA bank na Mastercard Tanzania umefanyika katika tawi la UBA Bank lililopo barabara ya Pugu huku baadhi ya wateja wa benki hio wakipata fursa pia ya kushuhudia uzinduzi huo wa huduma mpya ya kadi ya mastercard kutoka Bank ya UBA Tanzania.

Benki ya UBA Tanzania ambayo yenye matawi yake Posta, Kariakoo na Barabara ya Pugu huku ikiwa na mashine za kutolea pesa sehemu mbalimbali za jiji la Dar Es Salaam ikiwemo Segerea, Mikocheni, Mabibo na kwingineko.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu