Monday, June 26, 2017

UJUMBE WA SIKUKUU YA IDDI KWA WAISLAMU WOTE

Assalaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh. Ndugu zangu tuzingatie haya;

1. Swaum haijaisha.

2. Qur'an haijaondoka. 

3. Misikiti haijafungwa. 

4. Milango ya kujibiwa Dua haijafungwa. 

5. Malipo hayajakatika.

6. Kuweni wakumuogopa Allah,msiwe wa kuiogopa Ramadhani. Bimaana tuendelee kumuogopa Allah isiwe ndani ya Ramadhan tu. Na siku ya Idd Si yawale walovaa mavazi mapya,ila Idd ni wale wanao ogopa siku Ya Qiyaama, kutorudia maasi walo kuwa wakiyafanya mwazo.

Iddi Si yawale wa kijifukiza manukato mazuri Ila Idd ni yawenye kutubia Madhambi yao bila ya kuyarudia maasi. 

Iddi Sio yawale wenye kujinasibisha na wale Matajiri ila Iddi ni yawale kujinasibisha na wahali zachini.

Sio Iddi Kwa mwenye kujipamba na mapambo ya Dunia, hakika ya Iddi niyamwenye kujipamba na Pambo la Uchaji Allah. Ndugu zangu kaeni leteni Takbira, someni Qur'an na Nyiradi Mbalimbali msiende sehemu za Kumuaasi Allah S.W. JAZAAKUMULLAH KHEIR.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu