Friday, June 23, 2017

UNDP YACHANGIA MILIONI 110 HUDUMA YA MAJI KIKWAJUNI

Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akizungumza na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez(kulia) na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib, walipotembelea maeneo yatakayopita mabomba yakusamabaza maji kwa wakazi wa jimbo hilo.UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo.Picha zote na Abubakari Akida.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib,baada ya kumaliza kutembelea maeneo ya Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha mradi huo.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez,akifunga bomba la maji katika moja ya maeneo ambayo Mradi wa Maji Kikwajuni ushakamilika. UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akisadiana na Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto), kumtwisha mkazi wa jimbo hilo ndoo ya maji wakati wa ziara ya ukaguzi wa maeneo ulikopitia Mradi wa Maji Kikwajuni. UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha kukamilika kwa mradi huo katika maeneo yote ya jimbo hilo.Kulia ni Katibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya TAYI inayosimamia mradi huo, Abdallah Ahmed Suleiman.
Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez, akizungumza katika mkutano na wananchi wa eneo la Kikwajuni Mao, alipowatembelea baada ya kukagua maeneo unakopita Mradi wa Maji Kikwajuni ambapo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 110 kupitia UNDP kukamilisha mradi huo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni,visiwani Zanzibar, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kikwajuni Mao, katika mkutano huo aliongozana na Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez na Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.UNDP wameahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 za kitanzania kufanikisha Mradi wa maji katika jimbo hilo.
Mkazi wa Jimbo la Kikwajuni, Mohamed Seif Said, akijiandaa kumvisha zawadi ya kofia Mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez baada ya kuzungumza na wananchi katika mkutano uliohusu Mradi wa Maji jimboni hapo ambapo UNDP waliahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 110 ili mradi huo uweze kukamilika.Kulia ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Salama Abood Talib.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu