Sunday, June 4, 2017

VIONGOZI MBALIMBALI WAMIMINIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU DKT. PHILEMONI NDESAMBURO KUTOA POLE KWA FAMILIA

Maandalizo ya Mazishi ya marehemu Dkt. Philemoni Ndesamburo yakiendelea nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Kwaya ikihudumu kwa nyimbo kwa ajili ya kuwafariji wafiwa nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson akitoa mkono wa pole kwa mama Mjane wa Marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo alipotembelea nyumbani kwa marehemu kuifariji familia.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mjane wa marehemu Dkt Ndesamburo ,Ndehorio Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akitoa mkono wa Pole kwa mtoto wa marehemu Dkt Ndesamburo, Filomena Ndesamburo nyumbani kwao KDC mjini Moshi.
Waziri wa Malisili na Utalii, Prof Jumanne Maghembe akitoa pole kwa mama mjane wa marehemu Ndesamburo nyumbani kwake KDC mjini Moshi.
Baadhi ya watoto wa marehemu Philemoni Ndesamburo wakiwa nyumbani kwao.
Mbunge wa jimbo la Same Magharibi, David Mathayo David akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Philemoni Ndesamburo.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Idd Juma akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Ndesamburo KDC Mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Halmashauri wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) John Mrema akitia saini katika kitabu cha waombolezaji nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo KDC mjini Moshi.
Baadhi ya Madiwani wakitia saini katika kitabu cha waombolezaji.
Baadhi ya viongozi waliofika kutoa pole kwa familia ya marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mstaafu, NSaidi Meck Sadiki akisalimiana na Mwenyekiti wa Chadema taifa Freeman Mbowe walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo.
Saidi Meck Sadiki akitoa mkono wa pole kwa watoto wa marehemu Dkt Ndesamburo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akisalimiana na mume wa Mbunge wa viti maalumu Lucy Owenya ,Dkt Fidelis Owenya alipofika nyumbani wa marehemu Dkt Ndesamburo kutoa salamu za pole.
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Rombo Joseph Selasini walipokutana nyumbani kwa marehemu Ndesamburo.
Mjane wa marehemu Ndeamburo, Bi Ndehorio Ndesamburo (mwenye nguo za rangi nyeusi ).
Mwenyekiti wa Chadema Taifa na Kiongozi wa kambi rasmi Bungeni, Freeman Ndesamburo akisalimiana na Askofu wa KKKT Dkt. Martin Shoo alipofika nyumbani kwa marehemu Dkt Ndesamburo. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii -Kanda ya Kaskazini.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu